JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

MCC, yang’arisha miradi ya kijamii Tanzania

. Umeme wapewa kipaumbele

Mradi mkubwa wa ukarabati na upanuzi wa mfumo wa kusambaza umeme utakaohusisha mikoa 10, wilaya 24 na vijiji 356 Tanzania umezinduliwa hivi karibuni, ikiwa ni matunda ya Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC).

Wahadhiri TEKU watangaza mgomo

Hali si shwari ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), baada ya uongozi wa Chama cha Wahadhiri wa Chuo hicho (TEKUASA) na wanachama wake kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani ya kufunga mhula, inayotarajiwa kufanyika Julai mosi, waka huu.

LHRC: Tutazidi kumbana Waziri Mkuu

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Tanzania kimesema kitazidi kumbana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, afute kauli yake sambamba na kuwaomba radhi Watanzania.

‘Waliogawa mbegu mbovu Korogwe wakamatwe’

Katika kukomesha vitendo vya hujuma zinazofanywa na watendaji kwa wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo, amemwagiza Mkuu wa Polisi wilayani, Madaraka Majiga, kuwakamata watumishi wa Idara ya Kilimo waliosambaza mbegu mbovu za mahindi kwa wakulina na hivyo kuwasababishia hasara.

Tujifunze uzalendo, uchapaji kazi wa Wamarekani

Mwaka 2004 nilipata fursa ya kuzuru maeneo kadhaa nchini Marekani kwa muda wa takribani mwezi mmoja. Ilikuwa ziara nzuri. Nilijifunza mengi. Wasafiri wanasema kama hujafika Marekani, hujasafiri. Kauli hii inaweza kuwa ya kweli kwa sababu kuna mengi ya kustaajabisha na kutafakarisha – kuanzia kwenye maendeleo hadi tabia zao.

Mashabiki wa upinzani wajitazame upya

Tanzania ya leo inafuata mfumo wa vyama vingi. Katikati ya mfumo wa vyama vingi Watanzania wamegawanyika katika makundi makuu matatu.