Latest Posts
Ujio wa Obama wabadili mfumo Dar
Ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama, hapa Tanzania imebadili mfumo mzima wa matumizi ya barabara na shughuli mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Marekani ni fursa, Watanzania tuikumbatie
Taifa la Marekani limefika mahala sasa linaliamini taifa la Tanzania. Miaka ya 1960 na 1970 kutokana na Vita Baridi kati ya Marekani na Urusi, ilikuwa vigumu kwa Marekani kufanya kazi na Tanzania.
Marekani inavyoinufaisha Tanzania kupitia AGOA
Rais wa Marekani Barack Obama yupo hapa nchini kwa ziara ya kiserikali. Ujio wa Obama umekuwa na shamrashamra nyingi si tu Dar es Salaam bali macho na masikio ya Watanzania wote yameelekezwa katika safari hii. Ni ziara ambayo pamoja na mambo mengine mengi, pia imekusudia kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Maekani.
PPF yazidi kuchanja mbuga
Mfuko wa Pensheni za Mashirika ya Umma (PPF) umetangaza kuongeza fao la elimu kuanzia kidato cha nne hadi cha sita, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 35 ya mfuko huo.
BARACK OBAMA:
Rais wa Marekani wa tatu kuzuru Tanzania
Barack Obama anakuwa Rais wa Marekani wa tatu kuzuru Tanzania, ambayo imekuwa nchi ya kwanza kutembelewa na rais huyu katika ukanda wa Afrika Mashariki.
NUKUU ZA WIKI
Mwalimu Nyerere: Vyama vijihadhari kutumiwa
“Shughuli za demokrasia lazima ziwe kazi ya kudumu katika chama cha kidemokrasia na katika taifa la kidemokrasia, vinginevyo chama hicho wakati wote kitakuwa katika hatari ya kutumiwa na wakorofi wachache tu.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.