Latest Posts
Barua ya wazi kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo
Madudu, kero Hospitali ya Bagamoyo
Hivi karibuini nilikwenda kumjulia hali jamaa yangu aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo. Niliyoyaona yanashangaza sana kwa kuzingatia kuwa huko ni nyumbani kwa Mheshimiwa Rais wetu, Jakaya Mrisho Kikwete. Katika mantiki ya kawaida, kihuduma Bagamoyo ingekuwa ya kupigiwa mfano.
Obama atoboa siri
*Aeleza anavyokunwa na kazi nzuri inayofanywa na Tanzania
*Amsifia Rais Kikwete, aunga mkono Jeshi la Tanzania Congo
*Aeleza wazazi wake walivyoishi Tanzania, JK aishukuru USA
Rais Barack Obama wa Marekani ametua nchini na kupokewa kwa kishindo na kutoboa siri ya anayojua juu ya Tanzania, huku akieleza kuguswa na mapokezi ya aina yake.
Yah: Hili la makanisa nalo liangaliwe upya
Nianze kwa kusali Kikristo: Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe kama yanavyotimizwa huko mbinguni, utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe wanaotukosea, usitutie majaribuni…… ameni.
Vita ya uhuru wa Marekani
Vita ya Uhuru wa Marekani ilipiganwa kati ya Waingereza na walowezi wa makoloni yake 13 kwenye pwani ya Amerika ya Kaskazini katika miaka 1775 hadi 1783.
Jeshi la walowezi lililoongozwa na George Washington na wengine lilishinda Jeshi la Dola la Uingereza kwa msaada wa Ufaransa. Makoloni hayo yakapata Uhuru kama Muungano wa Madola ya Amerika au Marekani.
Vionjo vya marais wa Marekani
*Barack Obama: Mweusi wa kwanza kuiongoza
* Kennedy: Ndiye Mkatoliki pekee kukubalika
*Franklin: Alidumu muda mrefu madarakani
*William Henry: Aliongoza kwa siku 32 pekee
Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais wa Marekani ndiye mkuu wa nchi na Serikali ya Marekani. Ndiye mkuu wa Serikali ya Shirikisho, na ofisi ya rais ndiyo kubwa kiutawala nchini humo. Rais pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Marekani.
Utajiri wa Obama Sh bilioni 32
Dhana kwamba wanasiasa wanapaswa kuwa watu maskini huenda imepitwa na wakati. Rais wa Marekani, Barack Obama yeye na familia yake wanamiliki utajiri wa dola 19,225,070 sawa na Sh 31,529,114,800.