JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Utata wagubika mradi wa umwagiliaji Nyamboge-Nzera

Ndoto ya wakazi wa vijiji vya Nyamboge na Nzera katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ya kuendesha kilimo cha umwagiliaji imepotea.

FIKRA YA HEKIMA

LAAC imechelewa kugundua
madudu hazina, halmashauri

Ijumaa iliyopita, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ilitangaza kugundua mtandao wa wizi wa mabilioni ya shilingi za umma. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Rajab Mohamed Mbarouk, alisema mtandao huo unahusisha ofisi za Hazina na halmashauri mbalimbali hapa nchini.

Edwin Butcher: Hatuhusiani na Dk. Amani

Mmiliki wa duka la nyama linaloitwa Edwin Butcher la Rwamishenye, Bukoba, amejitokeza na kusema kuwa bucha yake haina uhusiano wowote na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Bukoba, Dk. Anatory Amani, au udini kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu.

Tiketi milioni moja zauzwa Kombe la Dunia

Shirikisho la Soka duninai (FIFA) limethibitisha kuwa zaidi ya tiketi milioni moja za Kombe la Dunia zimeombwa na mashabiki kupitia mtandao wake katika kipindi cha saa saba pekee tangu zianze kuuzwa.

Chelsea yaipokonya tonge mdomoni Spurs

 

Hatimaye Klabu ya Soka ya Chelsea ya Uingereza  imekubali kulipa kiasi cha pauni millioni 30 sawa na bilioni 75 za kitanzania, kumsajiliwa kiungo mchezaji Willian Borges da Silva,  kutoka klabu ya Urussi Anzhi Makhachkala.

TBS yadhibiti uharibifu injini za magari

Kuzinduliwa kwa mtambo mpya wa kupima mafuta kunaashiria kwisha kwa tatizo la muda mrefu la kuharibika kwa injini za magari yanayotumia mafuta ya petroli nchini. Mtambo huo wa kisasa uliozindulia wiki iliyopita na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda,  jijini Dar es Salaam, ni miongoni mwa mitambo inayopima mafuta ya magari iliyopo katika maabara ya kemia.