Latest Posts
Kambi ya upinzani walitoka na hoja zao
Wiki iliyopita, Mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa na vibweka na vimbwanga vingi vyenye kuacha kinywa wazi kwa mshangao na hamaki kwa mtu yeyote makini mwenye kuujali mustakabali mwema wa nchi yake.
Hata hivyo, pamoja na vibweka na vimbwanga vilivyotokea kwenye kikao hicho, ukweli unabaki kuwa kilikuwa kikao chenye moja ya miswada muhimu yenye kipekee unaokwenda kuweka jiwe jipya la msingi kwa Tanzania tunayoihitaji kuijenga kwa miaka 50, au hata 100 ijayo.
Hotuba iliyochafua hali ya hewa ndani ya Bunge
MAONI YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA SHERIA NA KATIBA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU KUHUSU
MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, YA MWAKA 2013
(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Huu ni Muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania. Kama Bunge lako tukufu litakavyokumbuka, Sheria hii ilifanyiwa marekebisho ya kwanza kwa kupitishwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Na. 2 ya mwaka 2012, mwezi Februari ya mwaka jana. Mabadiliko hayo ya kwanza yalihusu Sehemu ya Tatu na ya Nne ya Sheria hii, na yalilenga vifungu mbali mbali vinavyohusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba na utekelezaji wa majukumu yake.
Tanzania na biashara za kishirikina
Wiki iliyopita niliandika makala yaliyokuwa na kichwa, “Je kufanya biashara ni kipaji?” Ninafurahi kuwa yamekuwa makala yaliyowavutia wengi ambao hawakusita kunitumia mirejesho ya pongezi na maoni kupitia ujumbe wa simu, barua pepe na simu za miito. Msomaji mmoja amenitumia ujumbe ulionifurahisha kweli kweli; ninanukuu, “Makala yako ni nzuri na umechambua kitaalamu, lakini pia utajiri wa Wakinga asilimia 70 huwezi kuutenganisha na ushirikina. Vile vile Wachagga nao utajiri wao asilimia 30 ni ushirikina na 20% ni ujambazi. Na asilimia zilizobaki ndizo zinazoangukia kwenye uchambuzi wako,” mwisho wa kunukuu. Leo nitachambua kwa mara nyingine tena hili sekeseke la ushirikina kuhusishwa na biashara, si tu kwa Wakinga na Wachagga pekee, bali pia kwa wafanyabiashara wote bila kujali kabila wala eneo waliloko. Lakini kabla ya kuendelea na uchambuzi huu kwanza nina taarifa moja ya muhimu kwa wasomaji wetu.
Golikipa mwanamke ashinda tuzo Ujerumani
Golikipa wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Ujerumani, Nadine Angerer, ameshinda tuzo ya mwanamke bora mcheza soka barani Ulaya.
Vitisho vya Mahakama kwa gazeti Jamhuri
Septemba 3, mwaka huu, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Fakihi Jundu, aliitisha mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam na kutoa taarifa ifuatayo:
TAARIFA YA MAHAKAMA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HABARI ILIYOANDIKWA NA GAZETI LA JAMHURI; LIKIWATUHUMU WAH; MAJAJI NA MAHAKIMU KUWALINDA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA
Hivi karibuni imekuwa ni kawaida kusikia Majaji, Mahakimu au kesi mbalimbali zilizo mahakamani zikiendelea kusikilizwa, au maamuzi fulani yaliyotolewa na mahakama kulalamikiwa katika vyombo vya habari, na hatimaye watoe maamuzi husika au wasikilizaji wa kesi husika, ambazo nyingine huwa bado zinaendelea mahakamani kudhalilika na kuhukumika, na wakati mwingine, ushahidi kuharibika au kumshawishi Jaji au hakimu kutoa maamuzi kwa kufuata maoni ya magazeti, na ilhali maadili ya kazi za ujaji hayatoi mamlaka kwa walalamikiwa kujibu kwa kukanusha shutuma zilizo mbele yao kwa njia ya vyombo vya habari.