Latest Posts
Tumepoteza lengo la Siku ya Mashujaa
Katika kuwajali mashujaa waliopigania Uhuru na heshima ya Tanzania mwaka 1968, Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha TANU chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliamua kuweka siku maalum ya kuwaenzi mashujaa hao. Ikachaguliwa Septemba Mosi kila mwaka iwe Siku ya Mashujaa Tanzania.
KONA YA AFYA
Vidonda vya tumbo na hatari zake (7)
Wiki iliyopita, Dk. Ibrahim Zephania alizungumzia bakteria aina ya H. Pylori na madhara yake ndani ya tumbo la binadamu, na dawa ya vidonda vya tumbo. Sasa endelea kumfuatilia zaidi katika sehemu hii ya saba…
Sigara: Watu wanaovuta sigara/tumbaku ni rahisi kupata vidonda vya tumbo kuliko wasiovua, na vidonda vyao hupona polepole zaidi. Sigara huchoma kunyanzi za tumbo na kuzifanya ziwe rahisi kushambuliwa na asidi.
Katiba mpya iakisi uzalendo (3)
Sehemu iliyopita, mwandishi alisema Katiba nzuri ni ile inayokuwa na maadili ya kitaifa. Alieleza namna Katiba ya kwanza ya Tanganyika ambayo baadaye ilitumiwa kwenye Muungano wa Tanzania ilivyokuwa na misingi imara ya kulinda maadili ya nchi. Endelea
JAMHURI YA WAUNGWANA
Mungu tunamtwisha mizigo isiyomstahili
Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing, amesema kama kweli Watanzania wanataka kuondoka kwenye lindi la umasikini, waige kile kilichofanywa na nchi yake. Amesema China ya miaka 50 iliyopita ilifanana kwa kila hali na Tanzania ya wakati huo, ambayo imegoma (imegomeshwa) kubadilika. Imeendelea kuwa hivyo hivyo licha ya rasilimali nyingi.
FASIHI FASAHA
Miaka 50 hakuna maendeleo! (1)
Mengi yanasemwa, yanaimbwa na hata kubezwa eti hakuna maendeleo tangu nchi yetu ipate Uhuru wa bendera. Hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana kuinua maisha na mazingira bora ya mwananchi. Mtazamo huo una sura mbili kutokana na asili ya mazungumzo ya watu wanaosema, wanaoimba na wanaobeza. Sura ya maendeleo ya kwenda mbele na sura ya maendeleo ya kurudi nyuma. La msingi nani anazungumza na sababu gani ya kuzungumza.
FIKRA YA HEKIMA
Mishahara mipya isiwe kinadharia
Hivi karibuni Serikali imetangaza viwango vipya vya mishahara kwa watumishi wa umma, vitakavyoanza kutumika mwezi huu, ikitaja kima cha chini kuwa ni Sh 240,000. Mei 29, mwaka huu, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, aliliambia Bunge kuwa Serikali imekamilisha pia mchakato wa kuongeza kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi kitakachoanza kutumika rasmi Julai 1, mwaka huu.