JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Liverpool yamhitahi Manuel Iturra

Baada ya kuongeza Philippe Coutinho mwezi uliopita, Meneja wa Klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers, sasa anahitaji kuongeza kiungo mwingine, Manuel Iturra, kwenye kikosi chake.   Klabu ya Malaga ilisaini na kiungo huyo  msimu uliopita lakini mkataba huo ulifutwa mwishoni mwa…

Tanzania imejifunza nini AFCON 2013?

Mashindano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), yamehitimishwa Jumapili iliyopita huku Tanzania ikiwa mtazamaji na msikilizaji tu.

NUKUU ZA WIKI

 

Nyerere na matumaini ya wanyonge

“Bila Azimio la Arusha, wananchi wanyonge wa Tanzania watakuwa hawana matumaini ya kupata haki na heshima katika nchi yao.”

Haya ni maneno ya Baba wa taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

CCM wachimba umaarufu wa CHADEMA Moshi

MADIWANI wa Manspaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wamemwandikia barua Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakimuomba akubali kusaini makubaliano ya mkopo wa Sh bilioni 19 za ujenzi wa kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi kilichopo eneo la Ngangamfumuni mjini Moshi.

Unahitaji ‘gia’ ya uvumilivu kumudu biashara

Ninaandika makala haya baada ya kumtembelea Frank Mwaisumbe na kubadilishana naye mawazo, wiki mbili zilizopita. Ni mfanyabiashara aliyepo mjini Iringa anayemiliki kampuni ya uwakala wa safari za anga iitwayo Getterland Company Limited. Mwaisumbe pia ni mmoja ya waasisi wa Shirika la Mindset Empowerment linaloendesha mashindano ya mbio za Ruaha Marathon.

Wao na mashangingi, masikini na sakafu

Rais Paul Kagame wa Rwanda alipotwaa madaraka, miongoni mwa “uamuzi mgumu” wa awali aliouchukua ni kuhakikisha anapunguza matumizi yanayosababishwa na magari ya umma. Akayakusanya kwa wingi. Akayaweka uwanjani. Akapewa orodha ya maofisa na watumishi wanaostahili kukopeshwa magari. Akawaagiza waende uwanjani- kila mmoja achague analotaka. Akahakikisha aliyechagua gari anakopeshwa-linakuwa mali yake. Huduma za mafuta na matengenezo zikaandaliwa utaratibu kwa kila gari na kwa muda maalumu.