JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Nukuu ZA WIKI

Nyerere: Wafanyakazi wasinyonywe, waheshimiwe

“…wafanyakazi wa Tanzania wamelindwa wasinyonywe na matajiri wao, watu binafsi, na hata mashirika ya umma. Kila mfanyakazi apate heshima yake kama binadamu.”

Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere aliyasema haya kukemea unyonyaji dhidi ya wafanyakazi.

Yah: Yawezekana maendeleo au tumelogwa?

Siamini kama mtu ambaye anayemwamini Mwenyezi Mungu anaweza kuamua, kwa mkono wake, kukatisha maisha ya mtumishi wa bwana kwa moyo safi na wa kijasiri. Haya naona ni maendeleo mengine ambayo enzi zetu hayakuwako, sielewi kama napaswa kuwapongeza au kuwalaumu kwa maendeleo hayo.

Waraka wa uchumi kwa wafanyakazi

Leo nina neno kwa wafanyakazi waliopo katika sekta mbalimbali za umma na za binafsi. Nimeamua kuandika waraka huu wa uchumi kwa wafanyakazi kutokana na sababu kuu tatu. Mosi, uwepo wa mbinyo wa kuongezeka kwa gharama za maisha ikilinganishwa na vipato halisi vya wafanyakazi.

Tunaongoza kwa sikukuu nyingi zisizo na tija

 

Kufanya kazi ndiyo msingi wa maisha yetu ya kila siku, hususan jamii yetu ya Kitanzania ambayo wimbo mkubwa ni ukosefu wa ajira pamoja na ugumu wa maisha unaoongezeka kila kukicha.

fasihi fasaha

Serikali ishughulikie vurugu za kidini

Naungana na Watanzania wenzangu kulaani mauaji ya viongozi wawili wa dini ya Kikiristo yaliyotokea mkoani Geita na mjini Zanzibar, hivi karibuni. Aidha, natoa mkono wa tanzia kwa familia, ndugu na waumini wa dini hizo.

FIKRA YA HEKIMA

 

Tumeruhusu kucheka na nyani shambani, tutavuna mabua

 

Ni wazi sasa maji yanaelekea kuuzidi unga! Nchi yetu iko katika hatari ya ‘kuvuna mabua’ kufuatia kasumba ya kutoa mwanya wa ‘kucheka na nyani shambani’. Serikali na vyombo vyake vya dola vitabaki kulaumiwa, kwa kushindwa kudhibiti mfululizo wa matukio ya kutisha yakiwamo mauaji ya watu kikatili.