Latest Posts
JAMHURI YA WAUNGWANA
Kuanzia kitongoji hadi
Ikulu wote wanalalamika
Siku kadhaa zilizopita nilikutana na mwanahabari mwenzangu, Khalfan Said. Aliniuliza swali hili; “Huu uamuzi wa Rwanda na Uganda kususa bandari zetu utakuwa na athari gani kwa uchumi wetu.” Khalfan aliniuliza swali hili akitambua kuwa mimi si mchumi. Hilo analitambua vema. Mara moja nikatambua kuwa tunao kina Khalfan wengi wanaotaabishwa na jambo hili, kiasi kwamba wapo radhi kumuuliza yeyote wanayemwona hata kama wanajua si mtaalamu wa masuala ya uchumi.
Meya, mbunge Ilemela bado kunachimbika
Mgogoro baina ya Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mstahiki Henry Matata, na Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, unaendelea kufukuta na kujenga makundi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Hatujajipanga kuleta BRN katika elimu
Baada ya kuona kuwa wameboronga elimu na wameendelea kusemwa vibaya, sasa Waziri wa Elimu na wasaidizi wake wamekuja na jambo jipya kwa lengo la kujikosha. Wamekuja na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now-BRN).
Mchapishaji vitabu adaiwa kumdhulumu Halimoja
Mmiliki wa kampuni ya Educational Books Publishers ya jijini Dar es Salaam, anadaiwa kumdhulumu mwandishi mahiri na mkongwe wa vitabu nchini, Mzee Yusuf Halimoja. Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kwamba mwaka 2010 mchapishaji huyo wa vitabu na Mzee Halimoja walikubaliana kwamba mwandishi huyo aandike vitabu vya kiada vya masomo ya uraia na historia vya darasa la saba.
Waasi M23 wachapwa Goma
Brigedi ya Jeshi la Umoja wa Mataifa (MONUSCO) inayolinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, imewadhibiti waasi wa kundi la March 23 (M23). Brigedi hiyo inayojulikana kwa kifupi kama FIB, inaongozwa na Mtanzania, Brigedia Jenerali James Mwakibolwa. Kwa sasa imelidhibiti eneo la Goma.
Utata wagubika mradi wa umwagiliaji Nyamboge-Nzera
Ndoto ya wakazi wa vijiji vya Nyamboge na Nzera katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ya kuendesha kilimo cha umwagiliaji imepotea.