Latest Posts
Misitu inavyoinufaisha Nanjilinji ‘A’ (5)
Katika sehemu ya nne, Dk. Felician Kilahama alizungumzia kazi ya kutoa huduma bora za kijamii na kujenga miundombinu imara katika nchi yenye eneo kubwa. Alisema shughuli hiyo inahitaji ujasiri mkubwa na uzalendo wa hali ya juu. Sehemu hii ya tano na ya mwisho, Dk. Kilahama anatoa hitimisho.
Majaji wanaolinda wauza ‘unga’ wabainika
>>Gazeti hili sasa limeamua kuwataja kwa majina
>>Mahakimu nao wanawaachia mapapa kienyeji
>>Kigogo ofisi ya DPP, Mahakama Temeke, Kinondoni ni balaa
Mahakama kupitia baadhi ya majaji na mahakimu wasio waadilifu imebainika kuwa kikwazo kikubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini, uchunguzi wa JAMHURI umebaini.Pamoja na Mahakama, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP), nayo imelaumiwa kwa kufuta kesi katika mazingira ambayo hata mtu ambaye hakusoma sheria, anaweza kuyatilia shaka.
Wakati vyombo hivi vikikwamisha vita hii, lawama zimekuwa zikielekezwa kwa polisi na vyombo vingine vya usalama, ambavyo watendaji kazi wake wanafanya kazi usiku na mchana.
MISITU & MAZINGIRA
Misitu inavyoinufaisha Nanjilinji ‘A’ (4)
Pongezi kwa wananchi wa Nanjilinji ‘A’
Kwa kuzingatia mafanikio yaliyopatikana katika Kijiji cha Nanjilinji ‘A’ na kwa kuelewa kuwa mafanikio hayo yametokana na wanakijiji kudhamiria kwa dhati kutumia rasilimali misitu inayopatikana ndani ya mipaka ya kijiji chao bila kushurutishwa na mtu yeyote, napenda nichukue fursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwa uongozi wa kijiji na wakazi wake wote kwa mafanikio hayo ya kutia moyo.
Yah: Kazi kwanza, siasa ni kilimo si maneno
Mwaka 1974 katika rekodi ya vijiji bora Tanzania kwa kilimo, ufugaji na maendeleo ambavyo Julius alivipatia zawadi, ni pamoja na Kijiji cha Lwanzali kilichopo mkoani Njombe. Kijiji hiki kilipewa tangi kubwa la maji tena la chuma na mabomba yake ili kuunganisha maji kwa kila mwanakijiji.
KONA YA AFYA
Vidonda vya tumbo na hatari zake (10)
Wiki iliyopita, Dk. Khamis Zephania alielezea dalili za vidonda vya tumbo yakiwamo maumivu na tofauti yake kulingana na rika. Sasa endelea kumfuatilia katika sehemu hii ya kumi…
Tony: Nauza kahawa na digrii yangu
*Ni mhitimu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam
*Anauza kahawa stendi ya mabasi Ubungo
*Awaasa wasomi kutodharau kazi, aeleza mazito
Wakati vijana wengi waliohitimu elimu ya chuo kikuu wakikumbatia dhana ya kutarajia kuajiriwa serikalini na kwenye kampuni kubwa, hali ni tofauti kwa Tony Alfred Kirita, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).