Latest Posts
Rais Kagame si wa kumwamini sana
Makala iliyopita ya “JWTZ nginjangija Goma hadi Kigali’, imenifumbua macho. Nimepata simu nyingi na ujumbe wa maandishi usio idadi. Wapo waliotumia lugha kali, lakini wengi walikuwa waungwana. Hiyo ndiyo raha ya mijadala. Kuna wakati tunaweza kukubaliana kwenye baadhi ya mambo, na wakati mwingine tusikubaliane kwa hoja fulani fulani. Muhimu ni kujenga moyo wa uvumilivu na staha.
Sote tukiwa waoga nchi itayumba
Ni kosa kubwa kwa mtoto wa Kizanaki kumtamkia mtu aliyemzidi umri neno ‘mwongo’. Hawa ni tofauti na makabila mengine, mathalani Wajita. Wao mtoto ana uhuru na haki ya kumtamkia mzazi au mtu aliyemzidi umri neno ‘mwongo’. Wakati Mzanaki atapambana kumnasa vibao mtoto anayeamini kamtukana, mzazi wa Kijita atafanya juhudi za kupambana kwa hoja kumthibitishia mtoto yule kwamba yeye (mkubwa) si mwongo. Hizo ni tofauti za wazi kwa makabila hayo mawili.
Messi alipa faini ya kukwepa kodi
Nyota wa timu ya soka ya Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi pamoja na baba yake mzazi wamelipa euro milioni tano, sawa na dola milioni 6.6 za Marekani, baada ya kubainika na kosa la kukwepa kodi. Messi na mzazi wake huyo walidaiwa kukwepa kulipa kodi hiyo ya serikali kwa njia za ujanjaujanja.
Kambi ya upinzani walitoka na hoja zao
Wiki iliyopita, Mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa na vibweka na vimbwanga vingi vyenye kuacha kinywa wazi kwa mshangao na hamaki kwa mtu yeyote makini mwenye kuujali mustakabali mwema wa nchi yake.
Hata hivyo, pamoja na vibweka na vimbwanga vilivyotokea kwenye kikao hicho, ukweli unabaki kuwa kilikuwa kikao chenye moja ya miswada muhimu yenye kipekee unaokwenda kuweka jiwe jipya la msingi kwa Tanzania tunayoihitaji kuijenga kwa miaka 50, au hata 100 ijayo.
Hotuba iliyochafua hali ya hewa ndani ya Bunge
MAONI YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA SHERIA NA KATIBA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU KUHUSU
MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, YA MWAKA 2013
(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Huu ni Muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania. Kama Bunge lako tukufu litakavyokumbuka, Sheria hii ilifanyiwa marekebisho ya kwanza kwa kupitishwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Na. 2 ya mwaka 2012, mwezi Februari ya mwaka jana. Mabadiliko hayo ya kwanza yalihusu Sehemu ya Tatu na ya Nne ya Sheria hii, na yalilenga vifungu mbali mbali vinavyohusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba na utekelezaji wa majukumu yake.
- INEC yaboresha Daftari la Kudumu Mpiga Kura
- Meja Jenerali Martin Busungu afariki dunia
- Polisi wajipanga kuimarisha ulinzi na usalama msimu wa sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya
- CCM Tabora wamfariji mjane wa kada aliyejiua
- Chombo cha anga za juu cha NASA chajaribu kuweka historia kwa kuwa karibu zaidi na jua
Habari mpya
- INEC yaboresha Daftari la Kudumu Mpiga Kura
- Meja Jenerali Martin Busungu afariki dunia
- Polisi wajipanga kuimarisha ulinzi na usalama msimu wa sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya
- CCM Tabora wamfariji mjane wa kada aliyejiua
- Chombo cha anga za juu cha NASA chajaribu kuweka historia kwa kuwa karibu zaidi na jua
- NEMC yaonya kelele, uchafuzi wa mazingira wakati wa sikukuu
- Aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton alazwa hospitalini
- Israel yakiri kumuua Ismail Haniyeh
- Mwinyi: SMZ itaendelea kuleta mageuzi katika Mahakama
- Benki ya Dunia, SADC zampa tano Rais Samia
- Kuelekea msimu wa sikukuu wazazi, walezi watakiwa kuwajibika kwenye malezi ya watoto
- Tume zaundwa kuchunguza mgogoro wa ardhi, uhamaji kwa hiari Hifadhi ya Ngorongoro
- Soma Gazeti la Jamhuri Desemba 24 – 30, 2024
- RC Chalamila: Kuanzia Januari Kariakoo itakuwa masaa 24
- Jeshi la polisi Dodoma latoa mwelekeo wake msimu wa Sikukuu