JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Katibu Mkuu Nishati amwagiwa sifa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, amemwagiwa sifa kwa jinsi alivyowabana watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kufanikisha upatikanaji wa mita 85,000 za umeme.

Mkaa ni janga la kitaifa

Nimemsikia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, aliihoji Serikali ili ieleze mipango ya haraka ya kuokoa theluji katika Mlima Kilimanjaro.

‘Turejeshe Ujamaa, ubepari tumeshindwa’

Mkutano wa Nane wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma, umekuwa na michango mingi na yenye mvuto kutoka kwa wabunge mbalimbali. Ifuatayo ni sehemu ya michango hiyo.

Ukuaji wa deni la taifa udhibitiwe

Miaka mitatu iliyopita, deni la taifa lilikuwa Sh trilioni tano hivi, lakini mwaka huu wa 2012 deni hilo limepanda hadi kufikia zaidi ya Sh trilioni 20.

Waislamu wapuuzeni kina Ponda

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti, mwaka huu.

Mawaziri wagombana

*Naibu Waziri adaiwa kumhukumu Kagasheki wizarani

 *Atajwa kutoa matamshi ya kumkejeli huko TANAPA

*Waziri asema atamhoji, yeye asema  wanawachonganisha

 

[caption id="attachment_112" align="alignnone"]Waziri wa Maliasili na Utalii Khamis Kagasheki akiwa na Naibu wake, Lazaro Nyalandu kabla hali ya hewa haijachafuka[/caption]

MGOGORO mzito unafukuta ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ambapo sasa kuna msuguano mkali kati ya Waziri Khamis Kagasheki na Naibu wake, Lazaro Nyalandu.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Wizara hiyo, zinasema kuwa Kagasheki amepata taarifa kutoka kwa baadhi ya watendaji waliokuwa na watu mbalimbali walikuwa Arusha kwenye kikao alichokiendesha Nyalandu kati yake na maafisa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), alipomkejeli Kagasheki hivi karibuni.

“Katika Mkutano huo, Nyalandu alipoulizwa na wafanyakazi wa TANAPA juu ya hatua ya Waziri Kagasheki kusimamisha watumishi wanne wa TANAPA na askari 28, alisema ‘Waziri alikurupuka.’ Alisema ‘kama Waziri angeshauriana na yeye (Nyalandu) wala asingewasimamisha wafanyakazi hao,” kilisema chanzo chetu.