JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

‘Uhai wa raia unaangamia kwa kukosa ulinzi wa tiba’

UJUMBE WA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA KWA WAUMINI WAKATOLIKI NA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA

 

Sisi Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania tumekutana katika Mkutano wetu Mkuu wa 65 wa kawaida tangu tarehe 23-30 Juni 2012 uliowajumuisha Wakuu wa Mashirika ya Kitawa, wakuu wa Idara, Tume na Taasisi za Baraza pamoja na wawakilishi Walei.

 

La Dk. Ulimboka linahitaji uchunguzi huru

Tumemaliza wiki mbili sasa tangu litokee tukio la kinyama la kumteka, kumpiga na kumuumiza vibaya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka. Tangu litokee tukio hili baya na la kinyama, mjadala umekuwa mkali na yameibuka maneno ninayoamini yanapaswa kupatiwa majibu na uchunguzi huru.

Gandhi: Woga ni hatari

“Hakuna jambo baya linalomharibu binadamu kama woga, na yeyote anayemwamini Mungu anapaswa kujisikia aibu kwa kupata woga juu ya chochote [katika dunia hii].”

Haya ni maneno ya mpigania Uhuru wa India, Mahatma Gandhi aliyoyatoa wakati akiwahamasisha Wahindi kujenga mshikamano.

***

Weah: Mwanasoka aliyetamba dimbani, akatikisa katika siasa

Baada ya kumalizika kwa vita ya muda mrefu ya wenyewe kwa wenyewe huko Liberia, mwanasoka mstaafu, George Opong Weah, alitangaza kuwania urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, kisha akaanzisha chama kinachoitwa Congress for Democratic Change (CDC).

Tuwafundishe wasomi wetu kujiajiri

 

Miezi ya karibuni kule nchini Marekani askari walipambana na waandamanaji waliokuwa wakilalamika kuongezeka kwa pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho.

 

Mara kadhaa waandamanaji hao wamejaribu kuandamana kupitia njia mbalimbali, ikiwamo ile ya kukutana kwenye daraja la Mto Mississipi lakini mara zote wameambulia kufurumushwa na polisi.

 

Kashfa ya riba na vituko vya binti wa mkurugenzi

London ina upepo, ubaridi wa haja na mvua kwa siku mbili tatu hizi, lakini kuna wanaotokwa na jasho. Kihoro kimewashika wanene wachache, kwa sababu ya kashfa ya kupanga viwango vya riba za kukopeshana kwa benki za hapa.