Latest Posts
Ilikosewa kuruhusu UKAWA bungeni
Wiki iliyopita wanachama wa unaotajwa kuwa ni Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) walisusia kushiriki vikao vya Bunge Maalum la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma.
UKAWA hiyo inaundwa na wanachama wa vyama vya upinzani miongoni mwa wajumbe wanaounda bunge hilo lililokabidhiwa jukumu nyeti la kuwezesha upatikanaji wa Katiba bora ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi Bandari anahujumu Bodi
Uchunguzi uliofanywa na gazeti JAMHURI umebaini taarifa nyingi za uonevu katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Uonevu na ubabe wa Mkurugenzi, Madeni Kipande, haukuishia kwa wafanyakazi pekee, bali anaburuza hadi wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.
Hali hii inahujumu uchumi wa nchi. Baada ya kuona hatari inayolinyemelea Taifa, mmoja wa wakurugenzi aliamua kuwasilisha hoja ya kumuondoa Kipande madarakani, lakini kwa bahati mbaya kutokana na mizizi mizito aliyonayo Kipande, wenzake watano ndiyo walioondolewa kwenye Bodi, kwa Waziri Dk. Harrison Mwakyembe kuvunja Bodi hiyo na kuteua wateule awapendao. Ifuatayo ni taarifa husika katika tafsiri isiyo rasmi. Endelea….
Hofu yatanda Katiba mpya
*Ananilea: Rais akipenda ataokoa jahazi Wingu zito limetanda juu ya mchakato wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya viongozi wa dini na wanaharakati kutabiri kifo chake. Baadhi wamekosoa mfumo wa Bunge Maalum la Katiba, na…
Vibwanga vya Waziri Lazaro Nyalandu
*Madudu yake yanamchafua Rais Kikwete
Mara tu baada ya mawaziri wanne kujiuzulu na wengine kuondolewa kutokana na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza, mwandishi mmoja aliandika makala iliyokuwa inasomeka, “Kikwete ana mkosi gani na mawaziri wake?”
TCAA nako kwafukuta ufisadi
*Wakurugenzi wahariri Waraka wa Hazina
*Mbinu hiyo yawafanya walipane mamilioni
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), inakabiliwa na tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Fadhil Manongi, hadi wiki iliyopita bado alikuwa akiendelea na dhima za kiofisi licha ya muda wake wa kung’atuka kuwadia.
Wakati Manongi akijiandaa kuiacha ofisi hiyo, kumekuwa na malalamiko ya matumizi mabaya ya fedha miongoni mwa wakurugenzi ambao ni washirika wake.
Siku za Kipande bandarini zahesabika
*Ni baada ya kuthibitika anatumia vibaya jina la Rais Kikwete, Ikulu
*Amuagiza Mwakyembe amchunguze, wafuatilia kumtukana Balozi
* Mtawa, Gurumo nao wakana, Mwakyembe adaiwa kumwogopa
*Aendelea kukaidi maagizo ya Bodi, amng’oa rasmi aliyeomba kazi yake
Na Deodatus Balile
Siku za Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Mzee Madeni Kipande (58), kuendelea kuwa madarakani zinazidi kuyoyoma baada ya Rais Jakaya Kikwete kukerwa na tabia yake ya kutumia jina la Rais kuhalalisha matendo yake yenye kukiuka sheria za utumishi wa umma.
Habari za uhakika kutoka Ikulu na kwa baadhi ya mawaziri waandamizi, zinasema Rais Kikwete baada ya kupata taarifa za Kipande kutumia vibaya jina lake, alichukia na kuamua kumwita Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, na kumpa maagizo mazito.