JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Mjue Kada wa CCM Mohsin Abdallah

 

 

*Tume ya Jaji Warioba ilianika madudu yake

*Ni bilionea anayehodhi vitalu vya uwindaji

Hivi karibuni, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) aliuibua bungeni mkataba ulioingiwa baina ya kampuni za Uranium Resources PLC, Western Metals Limited na Game Frontiers of Tanzania Limited uliotengenezwa na Kampuni ya Kitanzania ya Rex Attorneys, na kusainiwa Machi 23, 2007.

Chonde chonde Malawi, ninyi ni ndugu zetu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ametangaza msimamo wa Tanzania kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya Taifa letu na Malawi. Kwa mara nyingine, Serikali kupitia kwa Membe imeitaka Malawi, kampuni na makundi mengine, kuacha mara moja kuendelea na shughuli za utafiti wa mafuta na gesi katika Ziwa Nyasa. Kama alivyosema, Malawi wanadai kwamba mpaka wa haki kati ya Tanzania na Malawi ni pwani ya ziwa hilo kwa upande wa Tanzania.

Twende Syria, liwalo na liwe

MOJA ya mambo ambayo huwa nawapendea baadhi ya viongozi wa Marekani ni msimamo wao kwenye mambo ya msingi. Sisemi kwamba viongozi wetu hawana msimamo la hasha, chonde chonde msinihukumu hivyo, lakini tangu zamani, kama si nguvu ya Marekani na maswahiba wake, wengi wangekuwa wameshaumia.

JWTZ wasogea mpakani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe, ameionya Serikali ya Malawi kuhusu mgogoro wa mpaka, katika kile kinachoonekana kuwa Tanzania ipo tayari kuingia vitani endapo itapuuzwa. Wakati Membe akitoa msimamo huo mkali bungeni jana, kuna habari kwamba wanajeshi na vifaa vya kijeshi wameshapelekwa karibu na eneo la mgogoro ajili ya kuimarisha ulinzi.

Rais Kikwete mbeleko ya mahakama ikikatika…

 

Taifa letu linakabiliwa na changamoto nyingi. Zimejitokeza changamoto ambazo kimsingi tunaweza kuondokana nazo. Sitazungumzia tishio la kitoto linaloelekezwa kwetu na taifa la Malawi. Binafsi sitaki kuamini kuwa mgogoro wa Ziwa Nyasa, ambalo Wamalawi kwa makusudi wanaliita Ziwa Malawi kwao ni mkubwa. Inawezekana Rais wa Malawi, Joyce Banda anatafuta umaarufu, lakini anaweza kuishia pabaya.

Haya mambo wakati mwingine yanahitaji kupata ushauri.

Nyerere: Wazanzibari waamue

“Ikiwa Wazanzibari wataukataa Muungano, bila mashinikizo kutoka mataifa ya nje, siwezi kuwapiga mabomu kuwalazimisha.”

Haya ni maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kueleza nia yake ya wazi kuwa ikiwa Wazanzibari wanaona hawautaki Muungano hawezi kuwazuia.