Latest Posts
NUKUU ZA WIKI
Nyerere: Umaskini wa fikra mbaya sana
“Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo (fikra), ni umaskini mbaya sana. Mtu mwenye akili akikwambia neno la kipumbavu ukalikubali, anakudharau.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
***
Nchimbi, Kagasheki, Sendeka hamjafanikiwa kumtetea Kinana
Wiki iliyopita mjadala mzito uliotawala hapa nchini, ni taarifa au tuhuma zilizoibuliwa na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa. Mchungaji Msigwa amemtuhumu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, kuwa anasafirisha pembe za tembo nje ya nchi.
Makali ya TBS yawatafunawenye viwanda feki
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limedhamiria kueneza uelewa, na kukuza matumizi ya viwango na kanuni za udhibiti wa ubora katika sekta za viwanda na biashara.
Uchumi ukikua, usiishie mifukoni mwa wabunge
Nimeishawahi kusema kwamba Watanzania tuna kumbukumbu dhaifu, kwa maana kwamba hatukumbuki jana na wala hatutaki kujua nini kitakachotokea kesho.
Mtanzania Mwenzangu, Yah: Madai ya Mei Mosi, sisi hatukuwa nayo?
Kuishi miaka mingi ni kuona mengi pia – lakini yanaweza kuwa mema ama machungu kama shubiri, lakini bado ni mambo muhimu katika mapito ya maisha ili kuweza kujifunza kila kitu. Nimejifunza mengi sana hadi leo.
Lissu: Tume ya Katiba ni ulaji
*Asema wanatumbua fedha, watengewa fungu la Ukimwi
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, wiki iliyopita aliwasilisha bungeni maoni ya Kambi hiyo, na kueleza namna Tume ya Mabadiliko ya Katiba inavyofuja fedha.