JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Nyerere: Ubovu wa CCM

“Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi.  Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha CCM kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao.”

Haya ni maneno ya Mwasisi na Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, wakati akiwahusia viongozi wa CCM kujirekebisha na kutumikia wananchi.

Kampuni za kigeni zinavyosulubisha za wazawa

Wakati fulani kule nchini Marekani kulitokea malumbano makali baina ya kampuni za Brother na Smith Corona zenye nguvu na ushindani mkali. Kampuni hizo zinajishughulisha na utengenezaji wa bidhaa zinazofanana zikiwamo mashine za kuchapa (typewriters), vichapishi (keyboards) za kompyuta, viyoyozi na vifaa lukuki vya kielektroniki.

Yanga ina jinamizi la saikolojia

Kila upande wa mabingwa wa kandanda Afrika Mashariki na Kati, Dar es Salaam Young Africans (Yanga) yenye makao yake makuu katika mitaa ya Jangwani na Twiga jijini, unaelekea kukabiliwa na jinamizi la kisaikolojia.

Zijue amri 10 za kujihakikishia umasikini milele

Mpendwa msomaji, najua juma lililopita vyombo vya habari vilitawaliwa na mauaji ya mwandishi Daudi Mwangosi. Nawashukuru wanahabari kwa mshikamano waliouonesha nchi nzima kwa maandamano, wanahabari tuendelee hivi hivi bila kutetereka.

Papa John Paul II: Mapadre si wanasiasa

“Ninyi ni wachungaji, si viongozi wa kijamii wala viongozi wa kisiasa. Hebu tujiepushe na mihemko itakayotufanya kuchanganya huduma ya Mungu na masilahi ya kupita yaliyotiwa chumvi.” Haya ni maneno ya Baba Mtakatifu Papa John Paul II alipokuwa akiwaasa wachungaji na…

Tanzania nako kuna 
Okwi, Bocco, Bahanuzi

Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inayodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, hatimaye imeanza Jumamosi iliyopita huku timu tatu za Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club mabingwa watetezi, Azam (Wanalambalamba) iliyoshika nafasi ya pili na Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ya mitaa ya Jangwani na Twiga, zote za jijini zikipewa nafasi kubwa ya kuitawala.