JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

TBS inavyojizatiti kuitekeleza sheria mpya ya viwango

• Yapania kutowaonea haya wazalishaji na waingizaji wa bidhaa hafifu

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1975, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekuwa likiwahudumia wananchi na umma kwa ujumla katika kuhakikisha kwamba ni bidhaa bora tu ndizo zinazoingia sokoni. Hata hivyo, kwa miaka mingi, utendaji wa shirika hilo umekuwa ukikwamishwa kwa kukosekana nguvu za kisheria za kuwachukulia hatua wale wanaokiuka kanuni na taratibu za ubora. Katika makala haya, MWANDISHI WETU anabainisha jinsi shirika hilo lilivyojizatiti kuitekeleza ipasavyo Sheria mpya ya Viwango ili kuhakikisha kuwa soko la Tanzania linatawaliwa na bidhaa bora…

Wakenya wamaliza msitu Tanga

*Maofisa wahusika wawakingia kifua

Hifadhi ya Msitu wa Mtae wenye ukubwa wa hekta 3,182 katika Tarafa ya Maramba, wilayani Mkinga, Tanga, iko hatarini kutoweka kutokana na uvamizi unaofanywa na raia wa Kenya, kwa baraka za baadhi ya viongozi na wananchi wa Tanzania.

WARAKA WA MIHARE

Waraka wa Mihale kwa Watanzania

Amani iwe kwenu wapenzi wasomaji wa Gazeti la JAMHURI. Karibuni katika safu mpya ya ‘Waraka wa Mihale kwa Watanzania’ itakayokuwa ikijadili mambo mbalimbali yahusuyo mustakabali wa nchi yetu.

Yah: Eti serikali tatu, hiyo moja tu matatizo

Wanangu, nianze kwa kuwashukuru kwa kuwa pamoja katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba mpya ya nchi yetu. Naiita katiba mpya kwa kuwa hatujawahi kuifuta tuliyonayo sasa isipokuwa tulikuwa tunaijazia viraka vya hapa na pale ili kufukia mashimo.

Mtuhumiwa Malele anaweza kuishitaki Polisi

 

. Ni kwa kumtangaza mgonjwa wa akili

Kijana aliyejitangaza kung’atuka ushirika wa mtandao uliohusika kumuua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, anaweza kulishitaki jeshi hilo kwa kumtangaza kuwa ni mgonjwa wa akili.

RASIMU YA KATIBA YA TANZANIA 2013

Hofu yatanda Z’bar

*Walio Tanganyika kugeuka wawekezaji

*Wasiwasi watanda, wanunua ardhi Bara

*Wahoji Tume ya Warioba kufuta Takukuru

Mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ya kuondoa suala la ardhi katika mambo ya Muungano, yamezaa hofu kwa Wazanzibari wanaoishi Tanzania Bara na ndugu zao walioko Zanzibar.