Latest Posts
Majibu kwa porojo za Nyalandu
Asoma na kujibu kiubabaishaji tuhuma kwenye magazeti aliyodai awali kuwa ni ya kufungia maandazi. Kwa muda mrefu sasa baadhi ya magazeti hapa nchini yamekuwa yakiujuza umma ukweli kuhusu Lazaro Nyalandu, ambaye kwa takriban miezi tisa sasa ni Waziri wa Maliasili na Utalii. Habari kumhusu Nyalandu zilianza kutolewa hata kabla hajawa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, wakati angali Naibu Waziri katika Wizara ya Viwanda na Biashara, chini ya Cyril Chami wakati huo. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakati huo alikuwa Joyce Mapunjo.
Balozi Mushi nakuunga mkono, ushoga hapana
Mpendwa msomaji natumaini hujambo kiasi. Nakushukuru wewe na wengine kwa ujumbe na mrejesho mkubwa mlionifikishia wiki iliyopita, baada ya makala yangu ya kuomba Watanzania tusifanye majaribio katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Hotuba iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 9, Desemba, 1978
Ndugu Wananchi,
Leo ni siku ya ambayo Tanzania Bara inatimiza miaka 17 tangu tumejikomboa na ukoloni. Kwa kawaida siku kama ya leo huwa tunafanya Gwaride Rasmi ambalo huwa lina linakaguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Wakenya waingiza mifugo Hifadhi ya Serengeti
Huu ni mpango mahsusi wa kuharibu utalii wa Tanzania na kuvutia watalii katika mbuga ya Maasai Mara nchini Kenya.
Rais chukua hatua, nchi inamalizwa
Watu wengi wameshtushwa na habari kwamba Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imetumia Sh bilioni tisa kwa ajili ya posho kwa kikao cha wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.
Mwekezaji alivyomvuruga Kamishna Madini
Mwekezaji katika migodi ya madini ya ujenzi, Majaliwa Maziku, anadaiwa kumlaghai Kamishna wa Madini nchini Tanzania, Paul Masanja, ili kufanikisha azma yake ya kupora ardhi ya wananchi kinyume cha sheria ya madini.