Latest Posts
Yah: Ugwadu na utamu wa tunda aujuae mlaji?
Nimesikiliza hotuba nyingi na za viongozi wengi walionona sura zao kwa maisha ya hali bora, wakijaribu kutuzungumzia walaji wa matunda ya umaskini na jinsi tunavyoteseka. Wote nawakubali lakini ni vema nikatoa tahadhari kuwa hayo maisha magumu wanayotuzungumzia wamehadithiwa hawayajui kabisa.
SALUM ABDALLAH Mwanzilishi wa Cuban Marimba
Mji wa Morogoro ni miongoni mwa miji iliyokuwa maarufu kwa michezo na burudani katika miaka ya 1950, 1960 na ya 1970.
Yanga iwe makini ili isimpoteze Jaja
Na Robert Mwandumbya
Genilson Santos Santana ‘Jaja’, ambaye kwa sasa ametawala vichwa vya vyombo vya habari, ameifungia Yanga mabao manne katika mechi tano alizocheza. Lakini taarifa nyingine zinasema kwamba katika mazoezi yaliyopigwa Uwanja wa Bandari, Loyola na kule Zanzibar, nyota huyo amefunga mabao zaidi ya 40.
Wenye akili wapo Ikulu!
Rais Jakaya Kikwete alipoamua kuleta suala la Katiba mpya kupitia ilani yake ‘mbadala’, wapo waliomshangaa.
Nakumbuka niliandika makala iliyosema, “Nitakuwa wa mwisho kuishabikia Katiba mpya”. Hiyo haikuwa na maana kwamba sikutambua wala kuthamini matamanio ya Rais wetu kuwaachia Watanzania Katiba nzuri!
Ahsante TMF, Kazi ipo kwetu
Miongoni mwa habari zilizopamba gazeti hili leo ni taarifa ya Mfuko wa Vyombo vya Habari nchini (TMF), kutoa ruzuku ya Sh. bilioni 1.7 kwa vyombo vya habari 16.Awali ya yote tunaupongeza mfuko huo kwa namna inavyoratibu shughuli zake na…
KWA HILI LA OKWI Yanga inahadaa mashabiki wake
Edgar Aggaba, mwanasheria wa Emmanuel Okwi, nyota wa soka wa kimataifa kutoka Uganda, hakufika Dar es Salaam kusimamia kesi ya mchezaji huyo wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilipojadili mkataba na usajili wake katika klabu ya Yanga.