JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Matusi kwa Rais wetu hayakubaliki

Kwa muda sasa, kumekuwapo maneno mengi kutoka kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda yakimlenga Rais wetu, Jakaya Kikwete. Chanzo cha yote haya ni mapendekezo ya Rais Kikwete ya kumwomba Rais Kagame aketi na waasi wa kundi la FNBL ili kukomesha mapigano na mauaji yanayoendelea Rwanda na upande wa mashariki kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Obama amedhihirisha ugaidi ni tishio

Tanzania imepata bahati ya kutembelewa na Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye ni miongoni mwa viongozi wakuu maarufu wachache duniani. Marekani ni taifa lenye nguvu kubwa ya kijeshi na kiuchumi. Ni miongoni mwa mataifa yanayounda Umoja wa G8 – yaani mataifa manane yenye nguvu za kiuchumi na kijeshi duniani.

Utajiri wa Loliondo na laana yake (3)

Sehemu iliyopita, mwandishi alieleza namna watu wa koo za Boroko la Loita kutoka Kenya walivyoingia Loliondo na kuonekana ndiyo wakazi halali wa eneo hilo. Anaeleza pia chanzo cha mgogoro Loliondo akisema ni vita ya uchumi ambayo sasa imepata kasi kutokana na raia wa kigeni na NGOs zinazofadhiliwa na mataifa ya Ulaya na Marekani. Endelea.

Ijue historia fupi ya Nelson Mandela

 

Nelson Rolihlahla Mandela ni Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini ya kidemokrasia. Ni mtu aliyejijengea heshima kubwa duniani kutokana na jitihada zake kubwa zilizofanikisha uhuru wa nchi hiyo na nyinginezo katika Bara la Afrika.

Hofu yatanda uwekezaji Kurasini

. Wanaohamishwa hawajui watakacholipwa

. RC Dar, diwani wawataka wavute subira

. Tibaijuka, Nagu watafutwa bila mafanikio

Hofu ya kuchakachuliwa fidia imetanda miongoni mwa wananchi wanaohamishwa kupisha ujenzi wa Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa katika Kata ya Kurasini, jijini Dar es Salaam.

MISITU & MAZINGIRA

Misitu ya Asili na Maendeleo ya  Jamii Tanzania (5)

Sehemu ya nne, Dk. Felician Kilahama alieleza namna wezi wa rasilimali za umma wanavyokwenda vijijini na kujitwalia maeneo ya misitu kwa mwavuli wa uwekezaji, lakini baadaye huishia kukata miti na kutoweka. Sehemu hii ya tano anaeleza namna vijiji vinavyonyonywa. Endelea