JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Malengo ya kazi (2)

Lazima wahakikishe kwamba kazi zote zinaendeshwa barabara, na pamba ya aina itakiwayo inapatikana na wakati ule ule inapoatakiwa; wahakikishe kwamba hakuna kipingamizi  kutoka hatua moja hata nyingine; kwamba kuna uhusiano baina ya kazi mbalimbali, na kwa sababu hiyo hakuna mfanyakazi anayekaa bure kungojea mwenzake amalize kazi yake.

Wakubwa wa kazi hawana budi kuhakikisha kwamba wananunua pamba ya kutosha, na kwamba wana mahali pa kuuzia nguo  zinazotengezwa; kwamba mishahara inalipwa bila ya kuchelewa;  kwamba hesabu ya fedha zinazowekwa sawa sawa; kwamba mitambo inakaguliwa ipasavyo; na mambo mengine kadha.

Wataalamu: Mtoto mpotevu Dar ana tatizo la kisaikolojia

Wanataaluma nchini wamesema kwamba wamefuatilia habari za kupotea na kupatikana kwa mtoto Happy Rioba (9), na kwa haraka wamegundua kwamba binti huyo ana tatizo la saikolojia tofauti na wengi wanaohusisha ushirikina.

Happy, anayeishi na mama yake, Sarah Zefania huko Mkuranga mkoani Pwani, aliripotiwa na vyombo vya habari kupotea na kupatikana zaidi ya mara moja, tukio lililovuta hisia za watu wengi.

Tugeukie mabadiliko ya Katiba, maandamano tuwe macho

 

Kumbukumbu zinanionesha sasa kuwa Watanzania wengi wanaamini kuwa suala la Katiba Mpya haliwezekani tena chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Ametafuta pa kutokea na kuamua kuelewana na wapinzani kupitia Kituo cha Demokrasia (TCD) na wakubwa hawa wakakubaliana yafanyike mabadiliko ya 15 ya Katiba.

Kwa mtego huu wa UKAWA hautamnasa Rais Kikwete

Tukio la hivi karibuni ambapo wajumbe wanaounda kundi la Umoja wa Katiba wa Wananchi (UKAWA) kuamua kuyakana makubaliano yaliyofikiwa baina yao na Rais Kikwete kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), haliwezi kupita bila kuhojiwa.

‘Utatu wa Maliasili’ ni wa ulaji

Watanzania tuna ugonjwa mmoja mbaya sana. Ugonjwa wa kutokuhoji lolote. Hatuna utamaduni wa kuhoji vitendo na kauli tata za viongozi na watawala wetu. Tumeridhika kuwa liwe liwalo; au yote maisha.

Kutokana na hali hiyo hatuna na hatuoni sababu za kuwawajibisha viongozi waongo, wazushi, matapeli na mafisadi. Matokeo yake viongozi na watawala hawa wamekuwa wakitumia udhaifu wetu wa kutokuhoji kufanya watakavyo.

Mbowe moto

.Adai moto aliowasha hauzimiki mpaka kieleweke 2015

.Asema anaumizwa kuteketea mamilioni Bunge la Katiba

.Atamba ipo siku polisi watazitambua haki za Watanzania

 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema anashangazwa na vigogo wa Jeshi la Polisi kufanya hila za kumkabili, ilhali wanaona namna Watanzania walivyodhulumiwa haki yao kupitia Bunge Maalum la Katiba.