JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

KAULI ZA WASOMAJI

CCM Rukwa tunataka serikali tatu

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Rukwa wamekwenda kinyume na msimamo wa chama chao na kutaka uwepo wa serikali tatu maana katiba ni kwa maslahi ya Taifa na sio wana CCM.

Ndugu wa Barlow wataka IGP Mwema awajibu

Ndugu wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow aliyeuawa kwa kupigwa risasi, wamesema wanataka majibu ya kina kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema.

MPOROGOMYI:

Waziri mstaafu aliyeanzisha kanisa

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Dk. Kilontsi Mporogomyi, ameanzisha kanisa. Kanisa hilo lenye Makao Makuu Makongo, linatambulika kwa Jina la Kanisa la Miujiza, Uponyaji, Kufunguliwa na Mafanikio.

FASIHI FASAHA

Miaka 50 hakuna maendeleo! -3

Katika makala mbili zilizotangulia nimeandika kuhusu kichwa cha habari hapo juu. Kwa maana kuwa baadhi ya viongozi na wananchi wa kawaida wanathubutu, tena bila haya, kupiga la mgambo kuwa eti miaka 50 hakuna maendeleo huku wanaendelea kuhamisha na kuiba mali na rasilimali za nchi kama kuwa ni haki yao na kupeleka nchi za nje.

Wakulima wa tumbaku waibiwa kitaalamu

Viongozi wa vyama vya ushirika mkoani Ruvuma, wanatumia hesabu za kisayansi kuwaibia wakulima mabilioni ya shilingi, hali iliyozaa mtafaruku mkubwa. Chama Kikuu cha Ushirika Songea, Namtumbo (SONAMCU) kimesambaratishwa baada ya viongozi kufukuzwa  uongozi katika vyama vya msingi kwa tuhuma ya kuwaibia fedha wakulima wa tumbaku.

JWTZ: Hizi ni rasharasha

*Wasubiri wenzao A. Kusini, Malawi zianze za masika

*Kamanda: Matumaini ya Wakongo ni makubwa mno

*Waziri wa Ulinzi asema hali za vijana nzuri

Brigedi ya Jeshi la Umoja wa Mataifa (UN) la Kulinda Amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) inayoongozwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ipo salama na inajiandaa usiku na mchana kuhakikisha amani inarejeshwa katika eneo hilo.

Habari za uhakika zinaeleza kwamba operesheni rasmi inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu baada ya vikosi kutoka Afrika Kusini na Malawi, kuungana na wenzao wa JWTZ ambao tayari wapo eneo hilo.