Latest Posts
NUKUU ZA WIKI
Julius Nyerere: Tusiruhusu wachache kuishi kifahari
“Kama watu wachache wanaishi maisha ya fahari fahari, na watu walio wengi hawapati hata mahitaji yao ya lazima, hatutaweza kudumisha amani na utulivu nchini mwetu. Ni muhimu sana kwa chama chetu na serikali yake kulizingatia jambo hili kwa makini.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Murray atolewa kombe la Rogers
Bingwa wa Wimbledon katika mchezo wa tenisi, Andy Murray ameshindwa katika mashindano ya mchezo huo baada ya kufungwa mpinzani wake Ernests Gulbis katika raundi ya tatu ya kombe la Rogers Cup mjini Montreal.
YITYISH AYNAW:
Mweusi aliyetwaa taji la Miss Israeli 2013
*Atimiza ndoto ya kukutana na Rais Obama
Ilikuwa Februari, mwaka huu wakati mrembo Yityish Aynaw (21), mzaliwa wa Ethiopia alipotwaa taji la ulimbwende la Miss Israel katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika nchini humo.
Wezi wa fedha za Smart Partnership washitakiwe
Kwa wiki kadhaa gazeti la JAMHURI tumeandika habari za ufisadi wa mamilioni ya shilingi kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Kimataifa ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue).
Malinzi: Uwanja wa Kaitaba unarekebishwa
Chama cha Soka mkoani Kagera kimewaondoa wasiwasi mashabiki wa mchezo huo mkoani humo kuhusu kasoro za Uwanja wa Kaitaba, kikisema unafanyiwa marekebisho uweze kutumika wakati wa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zitakazoanza hivi karibuni Agost 24 mwaka huu.
Mabaraza ya Katiba yadai uhuru wa habari
Leo kwa makusudi nimeamua nijadili mada hii sambamba na mada iliyotangulia hapo juu. Pamoja na matukio yanayoendelea ya uhalifu niliyoyajadili kwa kina kwenye safu yangu ya Sitanii, nimeona yaende sambamba na suala la Haki ya Kupata Habari.