JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

JK asifu utendaji wa Mchechu NHC

Rais Jakaya Kikwete ameusifu utendaji wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba (NHC), Nehemia Mchechu, kwamba  umerudisha heshima ya shirika hilo.

Ameisifu pia Bodi ya NHC, wafanyakazi wa shirika hilo kwa kutoa ushirikiano mzuri kwa mkurugenzi huyo.

Yah: Kama ningekuwa Waziri wa Usalama Barabarani

Wanangu, nawapa kongole ya kutimiza miaka 51 ya Uhuru mlionao hivi leo, nawapongeza kwa kuwa sisi wana-TANU ni kama ndoto ya kuamini kuwa tumeweza kuhimili vishindo vya wakoloni kwa kipindi chote hiki.

Sarafu moja Afrika Mashariki ni mtego

Wiki iliyopita hapa nchini umekuwapo mjadala wa kiuchumi, unaohoji mpango wa kuharakisha matumizi ya sarafu moja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mjadala huu umehusisha wadau mbalimbali, akiwamo Balozi wa Tanzania nchini Ubeligji, Dk. Diodorus Kamala.

DC Geita ageuka kituko

Mkuu wa Wilaya (DC) ya Geita, Manzie Mangochie, ameingia kwenye vita ya maneno na waandishi wa habari wilayani humo. Katika hatua ambayo haijapata kutekelezwa na DC yeyote, sasa Mangochie, anataka taarifa za waandishi wote, pamoja na sifa zao za elimu. Hoja yake ni kwamba anataka kuandaa “Press Cards”; jambo ambalo kwa miaka yote limekuwa likifanywa na Idara ya Habari (Maelezo).

Madudu mengine TTCL

*Wasaini mkataba wa ulaji wa Sh milioni 740 kwa mwaka

*Walishirikiana na maofisa kuweka ‘walinzi hewa’ lindoni

Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), imeingia mkataba wenye utata na kampuni moja ya ulinzi wenye thamani ya Sh milioni 742 kwa mwaka. Utadumu hadi mwaka 2015.

Fisadi wa madini huyu hapa

*Amejenga ghala Chang’ombe, kazi inafanywa kwa siri

*Huyavusha hadi Nairobi kwa kuyaficha kwenye ngoma

Mfanyabiashara mwenye asili ya kiasia, anaendesha biashara ya siri ya kusafirisha mchanga wenye madini kutoka migodini na kufanya uchenjuwaji katika ghala lake lililopo Dar es Salaam.