Latest Posts
Mtendaji mkuu Osha alalamikiwa Tughe
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dk. Akwilina Kayumba, amelalamikiwa mbele ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), kuwa anawaongoza kimabavu wafanyakazi wa taasisi hiyo ya Serikali.
Madudu ya mgodi wa Geita yaanikwa
Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) unadaiwa kukwepa kulipa kodi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kiasi cha Sh bilioni 38.2 tangu mwaka 2007 hadi 2013.
NUKUU ZA WIKI
Julius Nyerere: Tujifunze kusikiliza hoja za wengine
“Hatuna budi, hasa katika majadiliano na mazungumzo yanayohusu jumuiya, tujifunze kusikiliza hoja zilizotolewa na wenzetu, na kuzijibu kwa kuzikubali au kuzikataa, bila kujali kama aliyezitoa ni rafiki au si rafiki.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania.
Kamati Kuu CCM ikomeshe mgogoro unaofukuta Bukoba
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanajipanga kukutana wiki hii kutafuta ufumbuzi wa mgogoro mkubwa unaoendelea kufukuta katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera. Imeshadhihirika wazi kuwa mgogoro huo ni baina ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Meya Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani.
Dk. Mwakyembe sibipu, nakupigia mheshimiwa
Halo! Ni matumaini yangu kuwa uko hewani na unanisikia mheshimiwa. Nakuomba univumilie nimejiunga na mtandao wa Jamhuri kwa kuwa Voda, Tigo, Airtel na Zantel wameniambia salio langu halitoshi kuniwezesha niwe hewani kwa muda niutakao.
KONA YA AFYA
Misitu inavyoinufaisha Nanjilinji ‘A’ (3)
Mafanikio yaliyopatikana
Kijiji Nanjilinji ‘A’ kimedhihirisha kuwa iwapo wanavijiji watajipanga vizuri na kusimamia matumizi ya rasilimali ardhi na misitu ya asili katika vijiji, inawezekana kuboresha maisha yao. Kwa mtazamo wangu, Kijiji cha Nanjilinji ‘A’ kimekuwa mfano mzuri wa kuigwa na vijiji vingine vyenye rasilimali misitu, lakini misitu hiyo haitumiwi ipasavyo kwa faida ya wanakijiji. Kwa kipindi cha mwaka 2010/2011 kijiji kwa kushirikiana na MCDI kiliweza kupata soko la kuuza bidhaa za misitu hasa zitokanazo na mti aina ya mpingo.