JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Serikali yamkomoa msaidizi wa Mkapa

Kanali mstaafu Nsa Kaisi, ambaye amekuwa Msaidizi wa Rais Benjamin Mkapa kwa miaka mingi, amepokwa shamba lenye ukubwa wa ekari 14 katika eneo la Pugu Mwakanga mkoani Dar es Salaam.

Bosi TTCL ashinikiza mkataba wa mamilioni

*Asaini huku akijiandaa kung’atuka kazini

*Kampuni ya ulinzi yabainika utata mtupu

*Walinzi wake watuhumiwa wizi wa mali

MKATABA tata wa Sh milioni 742 kati ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Kampuni ya Ulinzi ya Supreme International Limited, umeanza kuwatokea puani viongozi wa TTCL, JAMHURI imethibitishiwa.

Kashfa kwa maofisa Ikulu

*Wadaiwa kukingia kifua waliotafuna fedha za wastaafu

*Msaidizi wa JK Mtawa abeba siri nzito, Katibu anena

*Mabilioni ya Hazina, bilioni 1.7 za NORAD zaliwa

Kashfa nzito inawazunguka watendaji wakuu wa Ofisi ya Rais Ikulu, wanaodaiwa kushirikiana na maofisa kadaa wa Hazina ama kutafuta fedha za wastaafu au kuwakingia kifua wabadhilifu.

Wasafirisha binadamu wahukumiwa Longido

Watanzania wanne wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kila mmoja, au kulipa faini ya Sh 5,000,000 kila mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la usafirishaji binadamu. Pamoja na adhabu hiyo, gari lililotumika kwenye biashara hiyo haramu limetaifishwa na litapigwa mnada.

Ujumbe wa mwaka mpya 2013 ulionivutia

Siku mbili kabla ya kuingia mwaka mpya nilipokea ujumbe kutoka kwa watu mbalimbali. Ujumbe huu ulikuwa wa kunitakia heri ya mwaka mpya mimi na familia yangu, lakini mwingine ulikuwa ukigusa masuala ya kitaifa na kimataifa. Nimepoke meseji nyingi, hivyo si rahisi kuziweka zote gazetini, isipokuwa hizi mbili tu nilidhani niziweke.

Kila kukicha aheri ya jana

Heri ya mwaka mpya wa 2013 wana-JAMHURI wenzangu, hongera na poleni kwa machovu yote.

Najua sana wengine ndiyo wanaangalia tena salio kwenye akaunti zao, kwenye waleti na chenji kwenye watoto wa meza nyumbani na ofisini.