Latest Posts
Safari hii ya Goma ihitimishiwe Kigali
Meja Khatibu Mshindo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amekufa katika mapambano nchini DRC. Amekufa kishujaa. Amekufa akitekeleza maelekezo halali ya Umoja wa Mataifa (UN) yanayolenga kuwafanya wananchi wa Mashariki mwa DRC waonje tunu ya amani. Kifo cha kamanda huyu kinapaswa kiwe chachu kwa Watanzania na wapenda amani katika Afrika na duniani kote.
Matakwa ya Rwanda yasiivunje EAC
Kwa muda wa mwezi mmoja sasa uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umezorota. Uhusiano huo umezorota baada ya matukio mawili. Tukio la kwanza ni ushauri Rais Jakaya Kikwete aliompa Rais Paul Kagame wa kuzungumza na waasi wa kundi la FDLR kwa nia ya kurejesha amani. La pili ni Tanzania kupeleka majeshi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupambana na waasi wa M23.
Matapeli wakubwa Tanzania hadharani
RIPOTI MAALUM
*Watumia madini kutapeli Wazungu hadi bilioni 160/-, watamba
*Mwanza, Dar, DRC, Zambia, Papa Msofe, Aurora waongoza ‘jeshi’
*BoT, NBC, Exim Bank, Polisi, Mahakama, Uhamiaji nao watumika.
Baada ya sifa ya Tanzania kuingia doa kutokana na watu wengi maarufu kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa matajiri wengi nchini wanatuhumiwa kufanya utapeli wa kutupwa kwa Wazungu kupitia ahadi hewa za kuwauzia madini.
Arsenal, Man City kibarua kigumu UEFA
Hali inaonesha kuwa timu za Arsenal na Manchester City huenda zikapata wakati mgumu kufuzu katika michuano ya hatua ya makundi ya Klabu Bingwa barani Ulaya (UEFA) kutokana na muundo wa makundi yanayozijumuisha timu hizo.
Bosi wa Masogange anaswa na ‘Unga’
*Anaswa na kilo 50 Nairobi, zinafanana na za wanamuziki
*‘Unga’ wagonganisha majaji, mahakamani watafutana
Wakati Mahakama Kuu ikituhumiwa kuharibu mwenendo wa kesi za dawa za kulevya nchini kwa kutoa hukumu zinazopingana na sheria zilizotungwa na Bunge, mtu anayetuhumiwa kuwa ndiye aliyewapatia mzigo wa kilo 180 za dawa za kulevya wanamuziki, Agnes Jerald (Masogange) na Melisa Edward waliokamatwa Afrika Kusini Julai 5, naye amekamatwa na ‘unga’.
Uhamiaji yamrejesha kwao wakala wa Kaseja