Latest Posts
Madudu ya Msekwa yaanikwa Ngorongoro
*Aliunda Kamati ikawa ndiyo Menejimenti
*Murunya naye ahusishwa kufaidi mabilioni
*Wameuza hadi mapitio ya wanyamapori
*Faru wengine watatu hawajulikani waliko
Timu ya ukaguzi iliyoundwa kukagua ‘madudu’ katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeanika ufisadi wa kutisha, JAMHURI inathibitisha. Spika wa zamani, Pius Msekwa, ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao ripoti hiyo imependekeza wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Msekwa ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo inayosifika kwa ufisadi.
M23 wafunga virago
*Kichapo cha JWTZ chawachanganya
*Wengine 1,000 wanaswa, waomba suluhu
*Kamati za Anna Abdallah, Lowassa zakutana
Sasa ni wazi kwamba waasi wa kundi la March 23 (M23), wamelewa kiasi cha kuomba mapambano yasimamishwe ili mazungumzo ya kuleta amani yaweze kutekelezwa. M23 wamelazimika kurudi nyuma baada ya kupigwa na Majeshi ya Umoja wa Mataifa (FIB) yanayoongozwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Kuna taarifa kuwa kwenye mapambano hayo, FIB waliwanasa waasi zaidi ya 1,000 na kuwanyang’anya silaha mbalimbali.
Yah: Sasa ndiyo nawakumbuka waliokuwa viongozi wazalendo
Huwa naona kama naota ndoto nzito, ambazo hazina mwisho kila ninaposikia vioja vya watendaji wa Serikali yetu katika kulitendea haki Taifa hili.
Napata taabu kukubaliana kama hawa ndiyo viongozi tuliowapigia kura ama walichaguliwa na Mungu, kuja kutuhukumu tungali hai kama vile mwisho wa dunia umefika.
IRENE DAVID: Binti aliyejiajiri kuuza matunda Dar
IRENE DAVID:
Binti aliyejiajiri kuuza matunda Dar
. Alikataa kutoa rushwa ya ngono aajiriwe
. Awaasa mabinti, wanawake wanaojiuza
Ni binti mrefu wa wastani, mwenye rangi ya maji ya kunde na umri wa miaka 23. Ni mhitimu wa kidato cha nne na fani ya kompyuta ngazi ya cheti, aliyejiajiri kuuza matunda. Binti huyu si mwingine yeyote bali ni Irene David, mkazi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam. Ana kawaida ya kutabasamu anapozungumza na mtu.
Hatuiaibishi Mahakama bali tunaijengea uwezo
Wiki iliyopita Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, ametoa taarifa ndefu kwa vyombo vya habari akilishambulia Gazeti la JAMHURI. Mashambulizi ya Jaji Kiongozi yalijielekeza katika msingi kwamba JAMHURI imekuwa ikifuatilia kazi za Mahakama, tena si kwa uzuri bali kwa kutafuta mabaya yanayofanywa ndani ya Idara hiyo.
MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE
‘Kutegemea kubaya kupita kote ni kutegemea mtu mwingine kwa mawazo