JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Ni chongo au kengeza?

Kuna msemo wa Kiswahili usemao ‘akipenda chongo huita kengeza’. Nimetoa msemo huu kwa nia njema tu ya kutaka kuangalia matukio kadhaa ya vurugu au ghasia, yanayotokea mara kwa mara hapa nchini na kusababisha baadhi ya watu wanaokuwa maeneo ya matukio kuumia, kujeruhiwa na wengine kupoteza maisha yao.

Mbio za Soweto Marathon matatani

Ugomvi umeibuka baina ya watayarishaji wa Mbio za Soweto Marathon nchini Afrika Kusini, wakisema hazitafanyika Novemba 3, mwaka huu.

Chameleon atwaa tuzo ya mwanamuziki bora Uganda

Msanii maarufu wa muziki nchini Uganda, Joseph Mayanja, maarufu kama, Jose Chameleon, hivi karibuni alitwaa tuzo ya msanii bora wa kiume wa kimataifa nchini humo. Chameleon ametwaa tuzo hiyo baada ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha Msanii Bora wa Kiume wa mwaka katika tuzo za Africa Entertainment Awards, zilizofanyika jijini Kampala, hivi karibuni.

Armstrong kurejesha medali IOC

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) inamsubiri mwendesha baiskeli wa Marekani aliyepatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini, Lance Armstrong, arejeshe medali ya shaba aliyoshinda kwenye mashindano ya Olimpiki ya mjini Sydney, mwaka 2000, amesema Mkuu wa Tume ya Sheria ya IOC.

Ufisadi Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro unatisha

Pamoja na malengo mengine ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), lengo mojawapo ni kuboresha miundombinu ya utalii ili kuboresha huduma za kitalii (to provide high quality tourism services) kwa kutengeneza barabara kwenda kwenye vivutio kama Nasera Rock, Olkarian Gorge na aina mbalimbali za miundombinu ya utalii na si kufanya kazi za Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Mkurugenzi: Wananchi Bukoba tulieni

*Asema ripoti ya CAG itatoa mwelekeo*Pande zinazovutana zaandaa ‘bakora’ Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Limbakisye Shimwela, amewaomba wakazi wa Manispaa hiyo kuwa watulivu na kusubiri majibu yatakayotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) baada ya ukaguzi…