Latest Posts
Madee – Nidhamu siri ya mafanikio
Msanii maarufu wa wa muziki nchini, Hamad Ally, maarufu kama ‘Madee’ (pichani) kutoka katika kundi la Tip Top Connection la Manzese, jijini Dar es Salaam, amesema kuwa siri ya mafanikio yake katika muziki ni nidhamu.
Nyerere alitabiri madhara ya uuzaji ardhi
Oktoba 14, mwaka huu Watanzania tuliadhimisha miaka 14 ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ifuatayo ni makala iliyoandaliwa na MWANDISHI WETU kwa msaada wa blogu ya Udadisi, ikielezea mtazamo wa kiongozi huyo kuhusu uzaji ardhi.
“Katika nchi kama yetu, ambamo Waafrika ni masikini na wageni ni matajari, kuna uwezekano mkubwa kwamba Mwafrika akiruhusiwa kuiuza ardhi yake katika miaka themanini au mia moja ijayo, ardhi yote ya Tanganyika itamilikiwa na matajiri wageni na wenyeji watakuwa watwana. Lakini hata kama wageni wasingekuwa matajiri, litaibuka tabaka la Watanganyika matajiri na wajanja. Tukiruhusu ardhi iuzwe kama kanzu, katika muda mchache kutakuwa na kundi dogo la Waafrika wakiwa na ardhi na walio wengi watakuwa watwana.” JKN 1958 (Uhuru na Umoja)
Mechi klabu bingwa Ulaya kuendelea leo
Wapenzi wa kandanda la Ulaya leo watakuwa na wakati mzuri wa kushuhudia mechi kadhaa za michuano ya soka klabu Bingwa barani Ulaya zikichezwa katika viwanja mbalimbali barani humo.
Ubovu viwanja vya soka usifumbiwe macho
Ligi kuu ya sokaTanzania Bara inaendelea katika viwanja mbalimbali hapa nchini. Hii ndiyo ligi kubwa hapa nchini ambayo imekuwa ikifuatiliwa na wapenzi pamoja na wadau mbalimbali wa soka nje na ndani ya nchi.
KIFO CHA NYERERE NI UTATA
Tangu mwaka jana juhudi za chini chini zilianza kufanywa na baadhi ya Watanzania ambao hawajaridhika kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alifariki kifo cha kawaida.
Michezo inapozidi kupoteza mwelekeo
Miongoni mwa vitu vinavyowavutia wapenzi wa michezo ni kuona nchi inasonga mbele kimichezo, kwa kufanya vizuri hadi ngazi ya kimataifa.