Latest Posts
Al-Shabaab wapo Tanzania
Matukio ya ugaidi yanayoendelea sehemu mbalimbali hapa nchini, yanathibitisha pasi shaka kuwa kundi la al-Shabaab la nchini Somali tayari lina makazi yake hapa nchini Tanzania.
Oktoba 7, mjini Mtwara walikamatwa vijana 11 wakifanya mafunzo ya ugaidi katika Mlima wa Makolionga wilayani Nanyumbu, na walikutwa wanamiliki silaha za moto, mapanga na DVD 25 zenye miongozo ya mafunzo ya al-Shabaab. Hii ilithibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen.
ADC: Dk. Shein anamuogopa Maalim Seif
Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimesema kitendo cha Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, kutomchukulia hatua za kisheria Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, kutokana na ofisi yake kutumia vibaya fedha za umma kinyume cha sheria, kimeupaka matope utawala wake na huenda anamuogopa kiongozi huyo.
Hukumu yamliza bibi kizee
Hukumu ya kesi ya rufani namba 285/2012 iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa Mkoa wa Mwanza, imemliza Bibi Kizee, Moshi Juma Nzungu (67), kwa hofu ya kunyang’anywa nyumba anayoishi tangu miaka ya 1957 katika eneo la Pasiansi, jijini Mwanza.
MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE
Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (7)
Wiki iliyopita tulichapisha sehemu ya sita katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, ambapo Mwalimu Nyerere anasema wazi kuwa baada ya kushauri ikashindikana, alirejea kijijini Butiama na kuamua kuandika utenzi. Leo, Mwalimu anasimulia nini kilimsukuma kuwaza kuwa uongozi wa CCM ulikuwa umepwaya wa kiwango cha kuhitaji nahodha mpya. “Hawawezi kutetea sera ya Chama ya Serikali Mbili wala mwelekeo wa Chama wa Serikali Moja. Watatumia uwezo walionao kutokana na hadhi walizonazo kuvuruga sera ya Chama na mwelekeo wake. Tutahitaji kiongozi mpya wa Serikali na kiongozi mpya wa Chama.” Endelea…DODOMA 12/11/1993
Nadhani uamuzi wa kuitisha kikao cha mchanganyiko ulifanywa na viongozi wetu katika kikao cha Dodoma II. Nimesema awali kwamba Waziri Mkuu alipohisi kuwa baadhi ya mawaziri wenzake walikuwa wanaunga mkono hoja ya Utanganyika na yeye kwa wakati huo alikuwa hajui aiunge mkono au aipinge, alipendekeza ifanyike semina ya viongozi wote ili jambo hili lizungumzwe na lipingwe nje ya Bunge.
Profesa Kapuya achunguzwe
Wiki iliyopita Taifa limetikiswa na habari za waziri wa zamani wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya, kutuhumiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 16.
BARUA ZA WASOMAJi
Madini yasichimbwe hovyo hovyo
Dhahabu ni Tanzanite, almasi na mali asilia nyingine nyingi huwa vinawekwa benki kuu kama sehemu ya fedha wanauchumi wananielewa Nyerere aliamua bidhaa kama hizi zisichimbwe hovyo hovyo benki kuu yake vibakie humo humo ardhi kwa kizazi cha baadae. Vipi wewe na mini unadhani tunanufaika kwa vyoyote vile na hizi bidhaa sasa zinachimbwa hovyo tokea Watanzania tusike kelele za gesi haijapita hata nusu mwaka tayari washasimika mabomba ya kuvuna Kuna uraniamu kule Singida nayo wanaifanyia mikakati ya kuichimba bila ya kuzingatia madhara ya kiafya itokanayo na uraniamu kwa kuzingatia kwamba hatuna wataalumu wazawa wa kutukinga mambo haya madhara ya uraniamu ni makubwa kuliko ukimwi.
0765441474