JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Jahazi Asilia: CCM, CUF wanahofu vivuli vyao

Chama cha Jahazi Asilia kimesema mtindo unaotumiwa na vyama vya CCM na CUF kubeba wanachama kwenda na kurudi kwenye mikutano ya hadhara hauvikisaidii vyama hivyo kujitambua na kupima kisiasa kama vinakubalika au la.

Dunia inalilia mawazo sahihi ya Mandela

Usiku wa Desemba 5, 2013 dunia ilipata habari mbaya. Nasema ilipata habari mbaya ambazo kimsingi zilitarajiwa, ndiyo maana sikutumia neno mshituko. Mzee wetu Nelson Madiba Mandela aliaga dunia.

MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE

Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (9)

Katika sehemu ya nane, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema Rais ndiye aliyekiri kosa la Zanzibar kuingia katika OIC na pili ndiye aliyelazimika kukiri kule Dodoma kwamba utaratibu wa kushughulikia hoja ya Utanganyika ulikosewa lakini mawaziri wake mara zote mbili walitulia tu nakumuacha Rais ndiye akiri kosa na kubeba lawama. Ifuatayo ni sehemu ya kitabu cha Mwalimu Nyerere alichokiandika mwaka 1994 cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Endelea…

 

Katiba ya nchi yetu, na utaratibu tunaojaribu kujenga, vinataka kuwa katika hali kama hiyo, Mawaziri ndiyo wawajibike, na hivyo kumlinda Rais, si Rais awajibike, na kuwalinda Mawaziri wake, na tena  kwa kosa ambalo si lake. Watu walioshindwa uongozi Bungeni, hata tukafikishwa hapa tulipo leo, ni Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa CCM.

Uhuru ulio wa kweli ni uhuru wa kiuchumi

Watanzania jana waliadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara). Maadhimisho haya yamekuja huku Afrika na dunia ikiwa katika simanzi kubwa kutokana na kifo cha Mzee Nelson Mandela (95), Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini.

KAULI ZA WASOMAJI

JAMHURI linatufaa kuhusu JWTZ   Hakika ni ukweli usiopingika kuwa habari zinazochapishwa kwenye Gazeti Jamhuri kuhusu vikosi vya askari wetu wa JWTZ wanaolinda amani nchini Congo zimekonga mioyo yetu na zimetuongezea shauku ya kulipenda jeshi letu, hasa sisi tuliopo mpakani…

Nazuiwa kumwona Jaji Mkuu Tanzania

Mhariri,

Nimekuwa nikifuatilia haki yangu katika mahakama kwa miaka 14 sasa bila mafanikio. Kwamba nimekuwa nikifanya jitihada za kuomba kukutana na Mheshimiwa Jaji Mkuu, lakini hadi sasa sijafanikiwa kutokana na kunyimwa nafasi hiyo na watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.