JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Kikwete, Warioba wako sawa

Na Christopher Gamaina Wiki iliyopita nchi yetu, Tanzania, iliweka historia ya kipekee. Rais Jakaya Kikwete kwa mara ya kwanza alihutubia wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ikiwa ni siku mbili baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini,…

Uchaguzi Chalinze ni huru, lakini si wa haki

Hivi karibuni nilishiriki mjadala unaohusu uamuzi wa Ridhiwani Kikwete kugombea ubunge Jimbo la Chalinze.

Kama ilivyo ada, mijadala ya aina hii mara zote imekuwa na mvuto. Kumekuwapo hoja kwamba wanaohoji uhalali wa mtoto wa Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge kupitia chama kinachoongozwa na babaake, ni wivu na husda!

Lakini wapo wanaoona kuwa kitendo hicho, ingawa ni haki yake ya kikatiba kama walivyo Watanzania wengine, hakiwezi kutolewa maelezo hata kikaweza kueleweka kwa wananchi walio wengi.

Sikukusudia kuendelea na mjadala huu kwa sababu tayari nilishaweka bayana faida na hasara za uamuzi wa Ridhiwani. Hata hivyo, makala kadhaa zilizoandikwa kwenye magazeti zimenifanya nirejee kutetea hoja yangu.

KAGAME NI MTIHANI

Viongozi Maziwa Makuu waufanye kwa uangalifu   Je, ulipata kujua undani wa kisaikolojia na mazingira-mali vilivyosababisha dunia kuingia kwenye Vita Kuu ya Pili miaka ya 1939-1945? Kama unajua karibu tutafakari. Kama hujui naomba nikueleze kwa kifupi. “Sera ya huruma iliyofanywa…

Bunge la Katiba livunjwe

Wiki hii Bunge linaanza mjadala wa rasimu ya Katiba. Mjadala huu unafanyika siku chache baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba, kuwasilisha rasimu hiyo bungeni, na baadaye Rais Jakaya Kikwete naye akalihutubia Bunge. Hotuba mbili za wakubwa hawa ndizo zilizonifanya niandike makala ya leo.

Sitanii, leo tunaumiza vichwa lakini chimbuko la matatizo yote haya liko wazi, ni Rais Jakaya Kikwete. Ibara ya 64 (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) inasema hivi: “Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Zanzibar kwa mujibu wa Katiba hii kuhusu mambo yote ya Tanzania Zanzibar yasiyo mambo ya Muungano, Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, Katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi inachokiuka Katiba itakuwa batili.”

Ibara ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatoa tangazo la nchi. Inasema Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano. Zanzibar mwaka 2010 walifanya mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, Ibara ya kwanza ya Katiba ya Zanzibar sasa inasema Zanzibar ni nchi.

Huu ulikuwa ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya Tanzania.

Kiwango cha ukiukwaji huu ni sawa na uasi au uhaini.

Ukaushaji sangara kwa moshi ni hatari

* Ni aina ya vibambara, wapakwa mafuta kuvutia wateja

*  Wakaushaji wanatumia nguo chakavu, pumba, plastiki

Ukaushaji wa samaki kwa njia ya moshi (kubanika) katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza na vitongoji vyake sasa unaanza kuwatia shaka walaji wa samaki hao na wataalamu wa afya.

Walaji wa samaki, hasa wa aina ya sangara (Nile Perch) na sato (Tilapia) ambao wanakaushwa kwa moshi katika Kanda ya Ziwa Victoria maarufu kama vibambara hawatayarishwi katika mazingira salama ya kiafya na mamlaka husika zinaelekea kutokuwa makini katika jukumu la kuhakikisha usafi na usalama wa chakula kwa walaji.

Samaki waliotayarishwa katika mazingira machafu wanadaiwa kuwa kisababishi cha maradhi kutokana na mazingira na vifaa vinavyotumika, ama kuwahifadhi, au kukaushia samaki hao.

Jiji la Mwanza, vitongoji vyake na baadhi ya visiwa vilivyo ndani ya Ziwa Viktoria ni maarufu kwa ukaushaji wa samaki. Kwa Jiji la Mwanza samaki wengi wanakaushwa katika Wilaya ya Ilemela, hasa majumbani na katika baadhi ya fukwe za wavuvi.

Zipo taarifa kwamba utayarishaji wa samaki wa kukausha kwa moshi unaweza kusababisha maradhi kwa watumiaji kama mambo kadha hayakuzingatiwa. Mambo haya ni kama vyombo vinavyotumika, kuwaosha samaki kabla ya kuwasha moto, mahali wanapohifadhiwa tayari kwa kukaushwa, aina ya kuni zinazotumika, muda wa ukaushaji, n.k.

Labda ukaushaji huo ungezingatia utaalamu huenda hatari hiyo ingeweza kuepukika kwa kiasi fulani, lakini uchunguzi wa gazeti hili umethibitisha ukaushaji wa samaki hao unaofanywa na baadhi ya wauza samaki kwa kiasi kikubwa unafanyika bila kujali afya za walaji.

Nyalandu ‘auza’ Hifadhi

*Yeye, James Lembeli waenda Afrika Kusini kukamilisha mpango 

*Baada ya Katavi Hifadhi nyingine nazo zitatolewa kwa wawekezaji

*Katibu Mkuu ashinikizwa, abaki njia panda kuidhinisha safari, malipo

*Urafiki wa Waziri, Lembeli waibua shaka miongoni mwa watumishi

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, yupo kwenye hatua za mwisho za kuikabidhi Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa mwekezaji wa Afrika Kusini.