Latest Posts
Kipande, Magesa wakoroga ICT bandari
Mamlaka ya Bandari Tanzania imegeuzwa sehemu ya ulaji wa hali ya juu. Hata hivyo, kutokana na mtandao mpana wa kuchota fedha unaoanzia wizarani hadi bandarini, yeyote anayetaka kuonesha paka yuko wapi, basi anaishia ama kufukuzwa kazi kwa njia ya vitisho, au kufanyiwa ‘kitu mbaya’.
Mkurugenzi Mkuu, Madeni Kipande, anamkingia kifua Mkurugenzi wa ICT, Phares Magesa, ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kuzamisha jahazi la bandari Tanzania.
Baada ya kuchapisha sehemu ya kwanza ya matukio yanayoendelea bandarini, wiki hii JAMHURI inakumegea sehemu tu kati ya madudu mengi yanayoendelea bandarini, ambayo kwa kila hali yanadhihirisha kuwa Mkurugenzi Mkuu, Madeni Kipande, ama hajui kitu kinachoitwa utawala wa sheria, au amedanganywa na watu wanaombeba pale Ikulu, hivyo amepoteza mwelekeo.
Ifuatayo ni sehemu ya barua ya ushauri wa kitaalamu, ambayo ilitolewa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi, Mei mwaka jana, akieleza hatari inayoinyemelea bandari kutokana na mfumo wa mawasiliano (Information and Communication Technology – ICT) kuchezewa katika Bandari ya Dar es Salaam na hivyo kupoteza mapato, imani ya wateja na kuhatarisha mizigo inayopitia bandarini.
Kwa mshango wa wengi, Dk. Jabir Bakari aliyeandika barua hii na kutoa ushauri, kwa mizengwe tu kama alivyosema Kipande kwenye kikao kati ya Wakurugenzi wa Bodi na Dk. Mwakyembe, Agosti mwaka jana huko Dodoma, kuwa “yeye ni mteule wa Rais na hivyo wakurugenzi hawambabaishi”, Kipande alifanya mbinu Dk. Jabir akafukuzwa katika Bodi ya Wakurugenzi wa Bandari kwa kutoa ushauri huu. Ifuatayo ni tafsiri isiyo rasmi ya barua hiyo. Endelea…
Nyalandu aanza kuliliza Taifa
*Marekani yapiga marufuku nyara kutoka Tanzania Uamuzi tata na wa kijazba wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, umeanza kuleta athari kwa tasnia ya uwindaji wa kitalii nchini. Marekani imepiga marufuku nyara zinazotokana na ndovu kutoka Tanzania kuingizwa nchini…
Wakubwa wanavyotafuna Bandari
Majambazi wajitangazia Serikali
*Wajiundia Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo
*Wabuni bendera, mahakama na polisi yao
*Vijiji vyawatii, waendesha ujangili, ujambazi
Watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 500 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na majangili, wamejiundia serikali ndani ya Msitu wa Igombe mkoani Tabora, JAMHURI inathibitisha.
Wamejiundia uongozi madhubuti pamoja na jeshi walilolipa jina la Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo.
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa huenda idadi ya watu hao ikawa kubwa kuliko inavyodhaniwa, kwani wanadaiwa kusambaa ndani ya misitu minene katika mikoa ya Tabora na Shinyanga. Pia wapo katika maeneo kadhaa ya Mkoa wa Kigoma.
Imebainika kuwa watu hao wapo katika Msitu wa Igombe uliopo wilayani Uyui na kusambaa katika mapori mengine ya Malagarasi na Myowosi; na walianza kujiimarisha tangu mwaka 2010.
Duru za uchunguzi zimebaini kuwa wanaounda ‘serikali’ hiyo wanatoka katika makabila kadhaa ya mikoa ya Tabora, Shinyanga, Arusha, Kigoma na katika mataifa jirani, hasa Burundi.
“Serikali” hiyo batili ina jeshi lake la ulinzi, jeshi la polisi, mahakama na vyombo vingine vya utawala.
Shughuli kuu zinazofanywa ni ujambazi, ujangili, kilimo cha bangi, biashara ya mbao, uuzaji bunduki pamoja na risasi; na uhalifu wa aina nyingine.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa, amezungumza na JAMHURI na kusema, “Ni kweli tuna tatizo hilo. Lipo na ni kubwa. Serikali imeshalitambua, na hatua zinachukuliwa.”
Mwasa, licha ya kukiri, hakutaka kuingia kwenye undani wa suala hilo katika kile kinachoonekana kuwa ni kutotaka kutibua hatua za kiusalama zilizopangwa kuchukuliwa na vyombo vya dola katika kukabiliana na genge hilo.
Hata hivyo, maneno ya Mwasa katika kuthibitisha ukubwa wa jambo hili ni haya, “Kweli tatizo lipo…ni kubwa kuliko unavyofikiri.”
Watu wawili waliokamatwa na baadaye kutoroka kutoka mikononi mwa kundi hilo wamesema genge hilo ni masalia ya wale walioshughulikiwa na Serikali mwaka 2010. Majina ya watu hao tunayahifadhi kutokana na sababu za usalama wao.
“Kuna jeshi lenye askari wa jadi wenye bunduki za SMG (Sub Machine Gun), na magobore. Wanaendesha uasi. Wamepandisha bendera ya bluu, imeandikwa Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo. Wahalifu wengi wageni wanatoka Burundi. Wanashirikiana na Wasonjo, Wasukuma na Waha.
“Shughuli zao ni kilimo cha bangi, kupasua misitu, uwindaji haramu na n.k. Wana watemi wao. Kila mtemi analindwa na askari wasiopungua 20,” anasema mmoja wa watoa habari wetu.
Uimara wa magenge hayo ya wahalifu yaliyojiimarisha yamewafanya hata wananchi na viongozi wa vijiji jirani na mapori wanamoishi, wawe watiifu kwao.
“Ukiwa na tatizo unaenda msituni kuomba msaada wa askari kukukamatia mhalifu au mbaya wako. Wanatumwa askari wanakuja kukuteka na kukupeleka huko msituni.
Bandari Dar inakufa
*Mkurugenzi Mkuu Kipande aingiza ukabila, udini, majungu
*Wafanyakazi watatu bandarini wafariki kutokana na vitisho
*CCTV hazifanyi kazi tangu 2011, wachonga dola mil. 6.5
*Mnikulu Gurumo, Mtawa wampa kiburi, wachafua jina la JK
*Amdanganya Dk. Mwakyembe, amtukana Balozi wa Japan
Kuna kila dalili kuwa Bandari ya Dar es Salaam inakufa kutokana na uongozi mbovu uliojiingiza katika majungu, udini, ukabila na majivuno yasiyo na tija. Wafanyakazi katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamepoteza morali wa kufanya kazi kutokana na vitisho na matusi ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Madeni Juma Kipande.
Hadi habari hii ya kiuchunguzi inachapishwa wafanayakazi watatu; Peter Gwamaka Kitangalala, Dotto Mbega na mwingine aliyefahamika kwa jina la Lyochi wamefariki dunia katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na shinikizo la damu lililozaa kiharusi baada ya vitisho vya Kipande.
Katika hali ya kuwavuruga wafanyakazi wa bandari, Katangalala alihamishiwa Mwanza na baada ya miezi miwili akahamishwa tena kwenda Lindi, huku akipewa vitisho kuwa muda wowote ajiandae kufukuzwa kazi. Kutokana na hofu, alipata kiharusi (stroke) akafa. Mbega kwa upande wake yeye alikuwa makao makuu Dar es Salaam, lakini kutokana na vitisho vya kila siku vya Kipande na wasaidizi wake, naye akapata kiharusi mwezi mmoja uliopita akafariki dunia.
Jumapili ya Machi 30, mfanyakazi mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Lyochi huku wengine wakisema ni Oluwochi mwenye asili ya Wajaruo, aliyehamishiwa bandari ya Kasanga, Sumbawanga naye aliaga dunia kwa ugonjwa huo huo wa kiharusi kutokana na mashinikizo ya Kipande.
“Uhalisia hali inatisha. Kipande anajinadi kuwa atamfukuza kila mtu, na kweli anafukuza anaajiri watu wa dini yake. Kuna kabila la Wahaya kutoka Kanda ya Ziwa, hilo utadhani waliwahi kushikana nalo ugoni. Mhaya yeyote aliyemkuta kazini ameapa kumg’oa. Amehamisha [Hassan M.] Kyomile kwa sababu ya kabila lake na kwamba aliomba kazi ya Ukurugenzi Mkuu,” kilisema chanzo chetu.
Kyomile amehamishwa Machi mwaka huu, kutoka makao makuu alikokuwa Mkurugenzi wa Ununuzi na kwenda kuwa Meneja wa Bandari Tanga.
Kikwete, Warioba wako sawa
Na Christopher Gamaina Wiki iliyopita nchi yetu, Tanzania, iliweka historia ya kipekee. Rais Jakaya Kikwete kwa mara ya kwanza alihutubia wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ikiwa ni siku mbili baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini,…
Habari mpya
- Bongo Movie kugusa jamii ya saratani
- Viongozi mbalimbali duniani wampongeza Trump
- Auawa kwa kukutwa na aliyekuwa mke wa mtu
- CCM: Uchaguzi Serikali za Mitaa kutumia 4R za Rais Samia
- Mkuu wa Jeshi Nigeria afariki
- Trump ashinda uchaguzi Marekani
- TRC : Kusimama kwa treni ya mchongoko ni hujuma
- Waziri Silaa mgeni rasmi mkutano wa nane wa Jukwaa la Wahariri kesho
- Bei za Mafuta mwezi Novemba 2024 zaendelea kushuka
- DAWASA yakutana na wananchi Msakuzi kupata hatma huduma ya maji
- Serikali yaeleza jitihada inazochukua kuwezesha matumizi ya gesi kwenye magari
- Mchango wa vyama vya siasa katika kumwezesha mwanamke kuwa kiongozi
- ‘Uchumi wa buluu una faida kubwa’
- Waziri Kombo atembelea maonesho ya kimataifa ya Biashara CUBA
- Chande azindua misheni ya uangalizi wa Uchaguzi ya SEOM jijini Port – Louis