Latest Posts
UKAWA mwaweza kuchagua vita, amani
Kwa muda wa miaka mitatu nchi yetu imeshuhudia mnyukano wa mchakato wa kupata Katiba mpya. Mnyukano huu ulianza rasmi mwaka 2011 Rais Jakaya Kikwete alipotangaza kuandikwa kwa Katiba mpya. Tangazo la Rais Kikwete lilianzisha mchakato wa kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo hatimaye imelifikisha taifa katika kupata rasimu.
Ukawa waigawa nchi
*Wagombe urais watarajiwa Pinda, Lowassa, Membe njia panda
*Marando, Lissu, Dk. Slaa wataka wananchi wapige kura ya maoni
* Kikwete, Prof. Lumumba, Jaji Mtungi wawataka warejee bungeni
Na Mwandishi Wetu
Kuna kila dalili kuwa Tanzania sasa iko njia panda baada ya msimamo usioyumba wa wabunge waliojinasibu kama Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kuwa hawarejei kwenye Bunge la Katiba linaloanza leo.
Ijue historia ya Kombe la Dunia
Katika kipindi hiki cha kuelekea fainali za soka za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil kuanzia Juni 12, mwaka huu, JAMHURI imeona vema kuwakumbusha mashabiki, wapenzi na wadau wa soka kwa jumla, historia ya mashindano hayo.
MANU DIBANGO: Gwiji la saxophone lililotimiza miaka 80
Manu Dibango ni gwiji wa kupuliza chombo adhimu katika ulimwengu wa muziki, kilichobatizwa kwa jina la ‘midomo ya bata’ (saxophone) na watu wa ‘mujini’, aliyejizolea sifa kemkem barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.
Nguli huyo Februari 10, 2014 alitimiza miaka 80 ya kuzalikwa kwake.
Jina lake halisi ni Emmanuel Dibango, ambaye, pamoja na kupuliza saxophone, pia ni mtunzi na mwimbaji mahiri mwenye sauti nzito.
Biashara ni wateja, tuwajali
Siku moja nilikuwa mji mdogo wa Ilula wilayani Kilolo katika mkoa wa Iringa. Nikiwa hapo niliingia kwenye duka moja la vifaa vya ujenzi nikiwa na lengo la kununua vifaa kadhaa vyenye thamani ya takriban shilingi laki tatu.
Katika duka hilo nilimkuta mama mmoja ambaye wakati akinipokea alionekana kuwa bize kubonyeza simu yake ya kiganjani. Nilipomsalimia hakujibu, na baada ya kuinuka kutoka katika kuitazama simu yake akaniuliza, “Nikusaidie nini?” Mimi nikamjibu kwa kumueleza vifaa ninavyovihitaji na kumuomba anitajie bei zake kimoja kimoja.
GERALD NYAISSA: Kijana msomi anayependa kujiajiri
*Hutumia makaburi kumwomba Mungu
Wiki iliyopita JAMHURI ilifanya mahojiano maalum na kijana msomi aliyehitimu elimu ya chuo kikuu katika fani ya utawala wa biashara. Huyu si mwingine yeyote bali ni Gerald Nyaissa, mkazi wa jijini Dar es Salaam.
Mahojiano haya yalijikita zaidi katika suala zima la kuchangamkia fursa za kujiajiri na kujijenga kiuchumi, badala ya kusubiri kuajiriwa serikalini na kupata misaada kutoka kwa wahisani. Yafuatayo ndiyo mahojiano yenyewe: