JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Watanzania tuchimbe madini yetu wenyewe

Awali ya yote namshukuru sana Mwenyezi Mungu ambaye kwa rehema zake nyingi anatuwezesha kuendelea kuwapo katika uso wa dunia hii.

Binafsi natambua kuwa nayaweza haya yote niyatendayo kila siku kwa sababu yupo mwenye uwezo kuliko wangu, na ndiye anitiaye nguvu na kuniwezesha ipasavyo kulingana na mapenzi yake.

Tanzania ijitoe Jumuiya ya Afrika Mashariki?

Katika toleo lililopita la gazeti hili, nilizungumzia hali halisi ya ujirani wa Tanzania na nchi nne nyingine zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki Tanzania.

Nilisisitiza kwamba katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Tanzania haina majirani wazuri. Nilitoa mfano wa Kenya ambayo imekuwa ikihujumu Tanzania na kuifanyia mambo ya uhasama yanayodhoofisha umoja na ushirikiano  wa Afrika Mashariki.

Kennedy Ndosi: Kina Ridhiwani wananivutia kuwania ubunge

 

Joto la Uchaguzi Mkuu mwakani, litakalohusisha ngazi ya urais, ubunge na udiwani, limepamba moto. Mmoja wa vijana, ambao wanaelekea moja kwa moja kuhitaji kulitumikia Taifa kisiasa ni Kennedy Elimeleck Ndosi, mtaalamu wa Ununuzi na Ugavi. Sifa kubwa ya Ndosi ni kutokukubali kushindwa kwa urahisi. Ni mpambanaji. Hii ni kwa sababu mtaalamu huyo wa ununuzi na ugavi ni mchapakazi. Ndosi ana ndoto za kuwa mbunge, na katika makala hii anajibu maswali katika mahojiano na mwandishi wa makala hii yaliyofanyika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam…

Tibaijuka: Nawapigania wasichana

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ameweka hadharani misaada na michango anayokusanya kwa ajili ya kuwakomboa watoto wa kike.

VITA DHIDI YA UJANGILI Waraka muhimu wa Mch. Matwiga …1

Ndugu Watanzania wenzangu na Wizara ya Maliasili na Utalii, kwanza naomba kusema jambo moja kama Mtumishi wa Mungu, ambaye nimeitwa naye kwa maslahi ya mbingu, ili kuijenga jamii na umma kimaadili. Nitasimama siku zote katika “kweli” na hiki ndicho “kiapo changu” ee Mungu tusaidie.

Wanaoiponda UDA wamekosa uzalendo

Tumetafakari kwa kina juu ya taarifa zinazolaumu “Serikali kubariki ufisadi wa UDA.” Lawama hizo hutolewa na Watanzania wachache sana wanaopinga Kampuni ya wazawa ya Simon Group kuuziwa hisa za UDA.

Hoja za msingi malalamiko hayo ni kwamba Simon Group haikufuata taratibu na sheria, na pia kwamba haikuzingatia thamani halisi ya shirika hilo. Tunachofahamu sisi kwa sasa ni kwamba uuzwaji huo uko sahihi na hakuna kinachoweza kubadilika, kwani taratibu na sheria zote zilizingatiwa kikamilifu wakati wa uuzaji wa hisa za UDA kwa Simon Group.