Latest Posts
Wanaokuzunguka wanaathiri mafanikio yako!
Nianze kwa kutoa taarifa. Katika toleo lililopita niliandika habari kuhusu Dk. Myles Munroe. Kuanzia Jumapili usiku na zaidi sana Jumatatu asubuhi ya wiki iliyopita, wengi walipata taarifa za kifo cha Dk. Munroe kwa ajali ya ndege.
Je, wafahamu maana ya neno ‘limited’?
Utangulizi
Ni kawaida unapopita mitaani au sehemu mbalimbali mijini au vijijini hasa kwa wingi kabisa katika miaka ya hivi karibuni, kuona maneno kama Company Limted. Sijui kama uliwahi kujiuliza maana ya neno hili Limited (Ltd).
Yah: Tanzania nchi ya viongozi kunukuuu na siyo kutekeleza?
Barua zangu kadhaa zilizopita nimekuwa nikijadili sifa na vigezo vya kiongozi ajaye na ambaye tunadhani anafaa kushika madaraka kwa Awamu ya Tano ya utawala. Nimetoa sifa ambazo kiongozi wa namna hiyo yupo japokuwa wengine watasema hayupo, lakini yupo tu lazima tukubali.
Watanzania tunaweza kufikia sifuri 3?
Kumbukumbu zangu zinanifahamisha ni miaka 25 sasa tangu mnong’ono wa kwanza kusikika mkoani Kagera kuwa kulikuwa na mgonjwa wa Ukimwi. Mnong’ono huo ukawa dhahiri ilipodhihirika kuwa kuna ugonjwa wa Ukimwi nchini, mwaka 1984.
Kama Muhimbili imeboreshwa, kwanini watibiwe ng’ambo?
Rais Jakaya Kikwete, anatibiwa nchini Marekani. Walimwengu wametangaziwa kwamba Rais wetu amefanyiwa upasuaji wa Tezi Dume. Naungana na wote wanaomtakia siha njema ili hatimaye arejee nchini salama.
Nyalandu chanzo cha Tanzania kutukanwa
Kwa mara nyingine tumeshuhudia Tanzania ikichafuliwa tena na kudhalilishwa na Wazungu mbele ya uso wa dunia. Safari hii wamarekani kupitia asasi ya Environmental Investigation Agency (EIA) wameibua aibu kubwa ya ujangili wakihusisha vigogo wa serikali yetu na Rais wa China.