JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Yah: Na mimi nataka ukuu wa wilaya siku moja?

NA BARUA YA S.L.P. Mzee Zuzu, C/O Duka la Kijiji Kipatimo, S.L.P. Private, Maneromango. Mtanzania Mwenzangu, Yahoo.com/hotmail.com/excite.com/www.http, Tanzania Yetu.         Kuna tetesi kwamba ukuu wa wilaya unagawiwa kama njugu na wanaosema hivyo labda wana taarifa kamili juu…

Kiwanda cha Sukari chafutwa uwekezaji

Wimbi la uingizwaji wa sukari nchini kwa njia ya magendo limeleta athari kubwa kwa viwanda vya ndani na baadhi yao sasa vimeanza kupunguza wafanyakazi pamoja kufuta baadhi ya mipango yake ya uwekezaji ya muda mrefu.

Mwaka mwingine wa kumkumbuka Mwalimu Nyerere

Katika sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amenukuliwa akiwasihi wanachama wenzake kuhimiza kujitokeza mgombea atakayeiletea CCM ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

Kuna ulimwengu mpya wa biashara 

Hivi karibuni nilikutana na bwana mmoja mtaalamu wa masuala ya kompyuta, aliyenishawishi na kunishauri niwe na “application” kwenye “google play”. (Nimeshindwa kupata Kiswahili cha “Google Play” na “Application”). Kwa kifupi huu ni mfumo unaopatikana kwenye simu za “Smartphones, tablet na iPads”, ambao unakuwezesha kuwasiliana na kufanya biashara.

Ukraine yaivuruga Urusi

Vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini Ukraine imeelezwa kutanuka na kusambaa nchini Urusi baada ya kiongozi wa upinzani, aliyepata kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Urusi, Boris Nemtsov, kupingwa risasi mwishoni mwa wiki.

Warembo wa India, Nepal watumikishwa ngono Dar

. Uhamiaji yawanasa Mwananyamala Kisiwani

. Yawaokoa, wasimulia mateso makali ya jijini

. Walikuwa ni watu wa klabu tu, hawalijui jua

. Waliambiwa hapo Mwananyamala ni ‘Sauzi’

. Warejeshwa kwao, waliowaleta waadhibiwa

. Sasa waziponza klabu za Continental, Hunters

. Raha ndani ya klabu hizo sasa ‘zaota mbawa’

 

Kwa kipindi cha miezi mitatu ya mwisho wa mwaka jana (2014), wasichana 22 kutoka nchi za Nepal na India, walitumikishwa ngono na kufanyiwa vitendo vya kinyume na haki za binadamu.