JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Arsenal, Man City kibarua kigumu UEFA

Hali inaonesha kuwa timu za Arsenal na Manchester City huenda zikapata wakati mgumu kufuzu katika michuano ya hatua ya makundi ya Klabu Bingwa barani Ulaya (UEFA) kutokana na muundo wa makundi yanayozijumuisha timu hizo.

Bosi wa Masogange anaswa na ‘Unga’

 

*Anaswa na kilo 50 Nairobi, zinafanana na za wanamuziki

*‘Unga’ wagonganisha majaji, mahakamani watafutana

Wakati Mahakama Kuu ikituhumiwa kuharibu mwenendo wa kesi za dawa za kulevya nchini kwa kutoa hukumu zinazopingana na sheria zilizotungwa na Bunge, mtu anayetuhumiwa kuwa ndiye aliyewapatia mzigo wa kilo 180 za dawa za kulevya wanamuziki, Agnes Jerald (Masogange) na Melisa Edward waliokamatwa Afrika Kusini Julai 5, naye amekamatwa na ‘unga’.

Uhamiaji yamrejesha kwao wakala wa Kaseja

 

Ni yule wa FC Lupopo ya Kongo

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imemrejesha rasmi, Ismail Baduka, ambaye alikuwa wakala wa golikipa namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Juma Kaseja, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ile ya kuishi nchini na kuendesha shughuli zake bila ya kuwa na kibali maalum.

TPSF: Tunataka sera ya kuwapendelea wazawa

Huenda Watanzania wataanza kunufaika ipasavyo na rasilimali za nchi, ikiwa Bunge litaridhia hoja ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) inayotaka ianzishwe sera ya upendeleo maalum kwa wazawa katika ugawaji zabuni na maeneo ya uwekezaji.

Bashar al-Assad: Mbabe anayeitikisa Dunia

 

Kwa zaidi ya miezi kumi nchi ya Syria imeingia katika mzozo uliosababisha machafuko makubwa nchini humo na kusababisha watu zaidi ya 1300 kupoteza maisha. Mzozo huo unasababishwa na wananchi wa nchi hiyo kutoikubali serikali inayongozwa na Rais Bashar al-Assad.

 

KAULI ZA WASOMAJI

Daraja la Mbutu vipi?

Pongezi kwenu waandishi wa Gazeti JAMHURI kwa kutujulisha habari zenye weledi. Kero yangu ni ujenzi wa daraja la Mbutu. Kasi ya ujenzi wa daraja hili umekuwa wa kusuasua, na masika karibu yanaanza. Jamani mnaohusika na ujenzi huu fanyeni haraka kuukamilisha