JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

NUKUU ZA WIKI

Julius Nyerere: Wanaotumia fedha kuomba uongozi hawatufai

Lindi, Mtwara wapata washirika Norway

Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo, na viongozi wa miji ya Hammerfest na Sandnessjoen nchini Norway, wamekubaliana kuanzisha ushirikiano baina ya miji hiyo na miji ya Lindi na Mtwara.

Yah: Al-Shabaab waishie huko huko walikoanzia

 

Kama miaka 10 iliyopita, hawa wenzetu Wakenya walikuwa na kazi kubwa ya kusuluhisha mgogoro wa uchaguzi, uliosababisha baadhi ya Wakenya kupoteza maisha na wengine kuendelea kuwa walemavu hadi leo.

 

Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania

 

‘Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania’ ni kitabu kilichoandikwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka 1994. Ndani ya kitabu hiki kuna maneno mengi makali na ya kukosoa uongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya wakati huo, iliyokuwa ikiongozwa na Rais Ali Hassan Mwinyi. Mwalimu aliwakosoa wazi wazi aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, John Malecela, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba. Ifuatayo ni sehemu ya kwanza ya kitabu hicho kama inavyoletwa kwenu neno kwa neno kama alivyoandika Mwalimu mwenyewe. Endelea…

Watanzania huu ndiyo ugaidi

Ndugu zangu nikiwa nawaza tukio baya la ugaidi lililotokea nchi jirani ya Kenya, punde napokea waraka kutoka kwa ndugu yangu Goodluck Mshana. Kipekee nianze kwa kuipa pole ya dhati Serikali ya Kenya na watu wake juu ya tukio la kigaidi lililotokea hivi karibuni. Aidha, niwapongeze wananchi wote wa Kenya kwa moyo wa kutoa pesa na damu kwa wapendwa wao.

Mr. Nice kujipanga upya

Soko la muziki wa Tanzania linakua siku hadi siku. Dalili za kukua kwa muziki zinadhihirishwa na ongezeko la wasanii wanaoibuka mara kwa mara. Hali hii imewafanya wasanii wakongwe na waliopata kuwika katika muziki kwa kiasi kikubwa, kufikiria kujipanga upya ili kuendana na soko la kisasa.