JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

TMF yaipa ruzuku JAMHURI

Wakufu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) umelipatia Gazeti la JAMHURI Ruzuku ya Mabadiliko (Transformation Grant) kwa ajili ya kufuatilia habari za uchunguzi. Gazeti la JAMHURI, limepata fursa ya kupewa ruzuku sambamba na gazeti jingine la Mwanahalisi, na redio nne…

Kodi za majengo, mimba za utotoni

Kwa muda wa wiki mbili sasa sijaandika katika safu hii. Nimepata simu nyingi, na ujumbe mfupi, wengi wa wasomaji wangu wakidhani kuna maswahibu yamenisibu. Nawahakikishia niko salama bin salimin na buheri wa afya. Sikuweza kuandika katika kipindi cha wiki mbili…

Atafuna mamilioni ya kijiji

Wananchi wa Kijiji cha Sango, Kata ya Kimochi, Wilaya ya Moshi Vijijini, wamepoteza mapato yanayofikia Sh milioni 60 katika kipindi cha miaka mitatu kutokana na fedha hizo kuliwa na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho. Wananchi hao wamelieleza JAMHURI kuwa fedha…

Ndugu Rais ‘walidhani nitakuwa nao’ tumaini lililorejea

Ndugu Rais, kama kuna wakati uligusa mioyo ya Watanzania na hasa masikini, ni pale uliposema, “Walidhani nitakuwa pamoja nao!” Kama hii ilikuwa ni ahadi, basi ni ahadi iliyotoka juu! Nina hakika hii haimo katika ilani ya chama chako. Kwa ahadi…

Yah: Nayaona mabadiliko yajayo kwa kasi isiyotarajiwa

Kuna wakati niliwahi kuandika katika waraka wangu kwamba kuna mabadiliko makubwa yajayo ambayo nayaona njozini, nilisema nikijihami kwamba labda ipo siku yanaweza kukwama, mkwamo ambao ungesababishwa na kusita kwa baadhi ya watu katika kutekeleza azma ya pamoja kukubaliana na kaulimbiu…

Madini ya Tanzania ni mali ya nani?

Nimepata kumsikia kiongozi mmoja wa siasa nchini akisema kuwa yanayotekelezwa na Rais John Pombe Magufuli kuhusu kudhibiti wizi na utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi, ni msimamo wake na ni ajenda ya chama chake cha siasa, ingawa chama chake…