JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Tuwaogope waporaji kwa kuwa ni Wazungu?

Wamarekani wanaweza kuwa na tofauti zao za ndani, lakini linapokuja suala linalohusu maslahi ya taifa lao huungana na kuwa wamoja. Ndivyo nchi inavyopaswa kuwa. Waasisi wa taifa letu walitambua thamani ya umoja na mshikamano wa wananchi. Wakautambua umoja kama moja…

Yah: Uamuzi wa kimkakati katika kila jambo ni roho ya mtu

Leo nimeamua kuanza na kauli hii kutokana na jinsi ambavyo uamuzi wa suala la makinikia lilivyovaliwa njuga na mkuu wa kaya na kuonesha wazi kuwa hakuna linaloweza kushindikana iwapo dhamira ya mtu binafsi inaweza kuamua kufanya jambo. Nimewaza mambo mengi…

Ngoma inakesha, isizimwe

Siku zilizopita, niliwahi kuzungumzia nafsi inavyoweza kutenda mambo mema au mabaya kutokana na binadamu anavyotaka. Naweza kusema kwa vile binadamu ameumbwa akiwa na silika; hali ya kujitambua na anapata uwezo wa kufanya lolote atakalo. Nafsi ni roho. Nafsi inayochungwa na…

Namna ya kuijua hati halisi kabla hufanya manunuzi

Ni wangapi wamefanyiwa utapeli katika harakati za kununua viwanja au nyumba. Ni wangapi wamepata hasara kubwa kutokana na michezo ya utapeli iliyotamalaki katika ardhi nchini. Ni kesi ngapi ziko mahakamani zinazohusisha utapeli katika mauzo na manunuzi ya ardhi. Idadi ni…

Watanzania mbona tunalumbana hivi? Tatizo liko wapi?

Kutolewa kwa ripoti ya kwanza ya makinikia kulizua mjadala mkali miongoni mwa Watanzania; kutolewa kwa ripoti ya pili kumemwaga mafuta ya taa kwenye moto uliyowashwa na mjadala uliotangulia. Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi uliofanywa na kamati ya rais iliyoteuliwa…

Ufafanuzi muhimu kuhusu usajili wa Acacia

Kwa kutumia kigezo cha usajili, Tanzania tunazo aina kuu mbili za kampuni. Kampuni za ndani (local companies) na kampuni za kigeni (foreign companies). Kampuni za ndani ni zile zilizoanzishwa hapa nchini na kusajiliwa hapa nchini. Hata kama wanahisa wake wote…