JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Namna ya kuishinda hasira yako (1)

Unaweza kutumia miaka 20 kujenga haiba yako mbele ya jamii lakini sekunde tano tu zinatosha kukiharibu kile ulichokijenga kwa miaka 20.                                                                                  Mtu mmoja alikuwa akisafiri kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Akiwa njiani kwenda Yeriko aliona kaburi moja limeandikwa: “Njia ya Mungu…

Uongozi Hospitali ya Amana haukumtendea haki marehemu

Kumetokea jambo ambalo nimejitahidi nibaki nalo moyoni lakini nafsi imegoma kabisa. Nafsi imegoma kwa sababu naamini kulinyamazia kutahalalisha matukio mengine mengi ya aina hii yaendelee kufanywa. Wiki iliyopita tulipata taarifa ya msiba wa mtu tunayemfahamu. Hana umaarufu, lakini ni binadamu…

Yah: Sheria zetu na namna ya kukabiliana na mazoea

Nianze na salamu. Najua kwamba tumeanza mwezi wa mwisho wa mwaka huu, ni vema tukatumia fursa hii kwanza kumshukuru Mungu kwa kutufikisha hapa tulipo. Pili, kama kampuni ya gazeti, tuna kila sababu ya kuwashukuru wasomaji wetu kwa kutuunga mkono, kwa…

Heshima ya kijana ni kazi 

Kijana na Ajira ni maneno mawili yenye maana tofauti katika istilahi ya lugha ya Kiswahili. Lakini ni maneno yenye uhusiano na ushirikiano mwema katika mazingira ya kufanya kazi ambayo huleta kipato kizuri na maendeleo mema kwa kijana. Kijana anapofanya kazi…

Si lazima mke kumtolea ushahidi mume wake

Mathalani, mume anatuhumiwa kwa kutenda kosa fulani. Upande wa upelelezi wakiwamo polisi na wengine wanaamini mke ni mtu pekee anayejua tukio, hivyo kuwa shahidi muhimu kwao. Au mke anatuhumiwa kwa kutenda kosa na mume ndiye mtu pekee anayeweza kuwa shahidi….

Drogba atundika daruga

Mchezaji nyota kutoka Ivory Coast aliyeng’ara akiwa na Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Didier Drogba, amestaafu kucheza soka baada ya miaka 20 ya hekaheka uwanjani. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 40, ameichezea Chelsea mara mbili tofauti na kufunga jumla…