Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Arusha, Richard Walalaze (35) amekutwa amefariki baada ya kujirusha kutoka ghorofani jijini Tanga.


Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe amesema kuwa mfanyakazi huyo amejirusha kutoka
ghorofa ya pili ya Hoteli ya Ocean Breez jijini Tanga alikokuwa amepanga chumba tangu
Julai 16 mwaka huu.

Imeelezwa kuwa Richard alikuwa miongoni mwa watumishi wa TRA waliokuwa jijini humo kwa kazi maalumu ya kuandaa taarifa ya Mamlaka hiyo ya mwaka.

JAMHURI MEDIA inaendelea kufuatilia taarifa zaidi juu ya tukio hilo, na tutakujuza punde tutakapofanikiwa.

Please follow and like us:
Pin Share