Kiongozi wa upinzani Raila Odinga anatarajiwa kuongoza maandamano nchini Jumanne.

Haya yanajiri baada ya Rais William Ruto kutia saini mswada Fedha 2023 na kuufanya kuwa sheria.

Kuporomoka kwa mazungumzo ya wanachama 14 ya pande mbili kati ya masuala mengine ndio yanayorejeshamuungano wa Azimio kwenye maandamano ili kushughulikia gharama ya juu ya maisha.

Maafisa wa Polisi wamesema wataruhusu mkutano wa leo wa Azimio kufanyika huko Kamukunji.

Inspekta Jenerali wa Polisi wa Nairobi Adamson Bungei amesema wametuma maafisa zaidi barabarani kwa usalama.

Amesema muungano huo umewaarifu kuhusu mkutano uliopangwa kufanyika katika Viwanja vya Kamkunji eneo la Muthurwa