Rais wa zamani Barack Obama anapongeza uamuzi wa Chuo Kikuu cha Harvard kukataa matakwa ya Ikulu ya White House ya kubadili sera zake au ikose ufadhili, katika ujumbe wake wa kwanza kwenye mtandao wa kijamii kukosoa utawala wa Trump tangu angalau Siku ya Kuapishwa.

Rais Donald Trump anazuia zaidi ya $2bn (£1.5bn) katika fedha za serikali kwa ajili ya Harvard kwa sababuimekataa kufanya mabadiliko katika uajiri wake, usaili na namna ya kufundisha ambayo utawala wake ulisema ni muhimu katika kupambana na chuki kwenye vyuo vikuu.

Obama, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Harvard, alielezea kuzuia fedha hizo kuwa “kinyume cha sheria”.

Alitoa wito kwa taasisi nyingine kufuata mkondo wa Harvard wa kutokubali matakwa ya Trump.