Barack Obama amemuunga mkono Makamu wa Rais Kamala Harris kuwa mgombea urais wa chama cha Democratic, na hivyo kumaliza uvumi kuhusu iwapo angemuunga mkono.

Rais wa zamani Obama na aliyekuwa Mama wa Taifa Michelle Obama walisema katika taarifa ya pamoja kwamba wanaamini Bi Harris ana “maono, tabia, na uwezo ambao unahitajika katika kipindi hiki kigumu”.

Bw Obama aliripotiwa kuwa miongoni mwa zaidi ya Wanademokrasia 100 mashuhuri, Bi Harris alizungumza nao baada ya Rais Joe Biden kutangaza Jumapili iliyopita kuwa anajiondoa katika kinyang’anyiro hicho.

Katika taarifa wakati huo, Bw Obama alipongeza kuondoka kwa Bw Biden, lakini hakumuunga mkono Bi Harris.

Makamu wa rais wa Marekani tayari amepata uungwaji mkono wa wajumbe wengi wa chama cha Democratic, na hivyo kumweka katika nafasi nzuri ya kuteuliwa rasmi katika kongamano la chama hicho mwezi Agosti.

Akina Obama walisema katika taarifa ya Ijumaa kwamba ni “furaha isiyokifani kumuunga mkono” Bi Harris. Waliapa kufanya “kila tuwezalo” kumchagua.

“Tunakubaliana na Rais Biden,” ilisema taarifa ya wanandoa hao, “kumchagua Kamala ilikuwa mojawapo ya maamuzi bora aliyofanya. Ana wasifu wa kuthibitisha kuwa anaweza.”

Walitaja rekodi yake kama mwanasheria mkuu wa California, seneta wa Marekani na kisha makamu wa rais.

“Hakuna shaka katika akili zetu kwamba Kamala Harris ana kile kinachohitajika kushinda uchaguzi huu na kutimiza matarajio ya watu wa Marekani.

Please follow and like us:
Pin Share