Na Isri Mohamed

Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Mulevya (DCEA), Aretas Lyimo amesema endapo nyumba yako au gari yako ikikutwa na dawa za kulevya, basi itataifishwa kwa mujibu wa sheria.

Kamishna Lyimo ameyasema hayo leo Novemba 25, 2024 wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo amewataka wamiliki wa magari na nyumba kuwa makini na mali zao.

Aidha ametoa wito kwa wamiliki wa nyumba za kupangisha kuchukua tahadhari kwa watu wanaowapangisha kwani wafanyabiashara wengi wa dawa za kulevya wamekuwa wakipanga nyumba kwa ajili ya kuhifadhi dawa za kulevya na wao kuishi sehemu nyingine.