Na Lookman Miraji, JamhuriMedia, Dar ea Salaam

MASHINDANO ya mchezo wa kuogelea kwa vijana yamemalizika hapo juzi kwenye bwawa la kuogelea lililopo katika Shule ya Kimataifa Tanganyika (IST) huku vijana mbalimbali wakichuana vikali.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili mara baada ya Ufunguzi wa michuano hiyo Rais wa Chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania (TSA), David Mwasyoge amesema amefurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na waogeleaji hao kutoka mikoa mbali mbi ya Tanzania Bara pamoja na Visiwani Zanzibar.

“Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika mashindano haya imetupa faraja kuona waogeleaji wadogo wamefanikiwa kuvunja rekodi zao kupitia mashindano hayo tunaamini miaka ijayo tutakuwa na timu bora ya Taifa,” amesema Mwasyoge.

Kwa upande wake. Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodgar Tenga ameema amefurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na waogeleaji hao.

“Nimefurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na waogeleaji hawa wameweza kuvunja rekodi zao vile vile wazazi wameonyesha ushirikiano mkubwa katika kusapoti vijana wao jambo ambalo linapaswa kuigwa na wengine, amesema Tenga.

Mwenyekiti huyo aliupongeza Uongozi wa Chama cha mchezo huo kutokana na juhudi kubwa wanayoifanya kuhakikisha mchezo wa kuogelea unazidi kukua.

Katika hatua nyingine Timu ya Taifa ya kuogelea Tanzania ya HPT imeweza kuipeperusha vema bendera ya Taifa kwa kushika nafasi ya tatu kati ya Klabu 30 zilizoshiriki kwenye mashindano ya Taifa yaliyomalizika Jumapili iliyopita Nairobi nchini Kenya.

Katika mashindano hayo muogeleaji Mark Tibazarwa ameibuka mchezaji bora na kuweza kupata medali mbali za shaba na mbili za dhahabu, wakati Romeo. Mwaipasi alipata zawadi ya mchezaji bora ambapo na medali nane ambazo kati ya hizo za dhahabu ni 7 wakati za shaba ikiwa 1.

Meneja wa timu ya HPT Francisca Binamungu alisema Crissa Dillip aliibuka mchezaji bora kwa upande wa wanawake baada ya kupata medali nane za dhahabu, na kudai pia amekuwa mshindi wa pili katika michuano ya mbio saba.

“Kwa kweli tunajivunia mafanikio tuliyoyapata waogeleaji wetu wametutoa kimaso maso kwa kufanya vizuri kwenye mashindano hayo yaliyokuwa na upinzani mkubwa, alisema Binamungu.

Aidha alisema Delbert Kanemo naye amefanikiwa kupunguza muda katika mbio zake zote alizokimbia.

Mwishooo.

Please follow and like us:
Pin Share